NA K-VIS BLOG, LEADERS CLUB
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, ameshiriki katika michezo
ya “Waajiri Health Bonanza” kwenye
viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2023.
Bonanza hilo lililoandaliwa na Chama cha Waajiri
Tanzania (ATE) lilikwenda sambamba na maonesho yaliyoshirikisha taasisi za umma
na binafsi ambapo washiriki walipata fursa ya kupata huduma mbalimbali.
Miongoni mwa taasisi zilizokuwa zikitoa huduma ni pamoja
na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambapo baadhi ya
washiriki ni wanachama wake.
Mhe. Profesa Ndalichako ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye bonanza hilo alitembelea kwenye mabanda mbalimbali ili kujionea shughuli zilizokuwa zikiemdelea.
Moja ya mabanda aliyotembelea ni banda la PSSSF, ambapo alipokelewa na Bi. Mercy Nzaga Shumbusho, Afisa Mwandamizi, Huduma kwa Wateja, PSSSF, ambaye alimueleza huduma walizokuwa wanatoa kwa wanachama waliofika kwenye banda hilo.
Bi. Shumbusho alimueleza Mhe. Waziri, kuwa walitoa elimu ya namna ya kutumia huduma za PSSSF Kiganjani Mobile App ambapo mwanachama atapata huduma
kupitia simu yake ya mkononi na PSSSF
Ulipo Mtandaoni Member Portal ambapo mwanachama atapata huduma kupitia
tovuti ya Mfuko na waajiri kuweza kulipa michango na kujihudumia wenyewe yaani self-services.
Viongozi wengine waliohuduria bonanza hilo ni pamoja
na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vinjana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Mhandisi Cyprian Luhemeja, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama
Cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Suzanne Ndomba, Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA), Bw. Henry Mkunda na Wakuu wa taasisi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.
Profesa Joyce Ndalichako, akihutubia washiriki wa “Waajiri Health Bonanza”
kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2023