Mkuu wa Kanda ya Kati wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Bw. Joseph Sayi (kushoto) akikabidhi msaada wa madawati kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Medeli A, Bw. Daniel Atilio ikiwa ni sehemu ya jitihada za msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama uliodhaminiwa na asasi ya Vodacom Tanzania Foundation. Waendesha baiskeli takribani 200 walianza safari yao jijini Dar es Salaam Oktoba mosi na wanatarajia kufika Wilayani Butiama Oktoba 14 ikiwa ni juhudi za kuenzi maisha na urithi wa Mwalimu Nyerere kupitia utekelezaji wa shughuli za elimu, mazingira, na afya.
Mkuu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati, Bw. Joseph Sayi (wa pili kushoto) akiwa ameshikilia mche wa miti pamoja na Mwenyekiti wa Twende Butiama, Bw, Gabriel Landa kushoto kwake ikiwa ni sehemu ya jitihada za msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama uliodhaminiwa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation. Waendesha baiskeli takribani 200 walianza safari yao jijini Dar es Salaam Oktoba mosi na wanatarajia kufika Wilayani Butiama Oktoba 14 kama juhudi za kuenzi maisha na urithi wa Mwalimu Nyerere kupitia utekelezaji wa shughuli za elimu, mazingira, na afya.
Baadhi ya waendesha baiskeli wa msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama uliodhaminiwa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, wakiwa na wanafunzi wa Shule ya msingi Medeli A ya jijini Dodoma ambapo waliweka kituo na kushiriki shughuli za upandaji wa miti na kukabidhi msaada wa madawati. Waendesha baiskeli takribani 200 walianza safari yao jijini Dar es Salaam Oktoba mosi na wanatarajia kufika Wilayani Butiama Oktoba 14 kama juhudi za kuenzi maisha na urithi wa Mwalimu Nyerere kupitia utekelezaji wa shughuli za elimu, mazingira, na afya.
Baadhi ya waendesha baiskeli wa msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama uliodhaminiwa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, wakiwa katika picha ya pamoja katika mnara wa Mwalimu Nyerere jijini Dodoma ambapo waliweka kituo na kushiriki shughuli za upandaji wa miti na kukabidhi msaada wa madawati Shule ya msingi Medeli A. Waendesha baiskeli takribani 200 walianza safari yao jijini Dar es Salaam Oktoba mosi na wanatarajia kufika Wilayani Butiama Oktoba 14 kama juhudi za kuenzi maisha na urithi wa Mwalimu Nyerere kupitia utekelezaji wa shughuli za elimu, mazingira, na afya.