MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA KIKODI WA ARUSHA OKTOBA 03, 2023 IMEWATEMBELEA WAZALISHAJI NA KUFANYA UKAGUZI WA BIDHAA ZINAZOBANDIKWA STEMPU ZA USHURU WA BIDHAA KATIKA MKOA HUO
TIMU HIYO MAALUM YA UKAGUZI IKIONGOZWA NA AYUBU TWEVE MENEJA WA ETS PAMOJA NA EVA RAPHAEL MENEJA WA MKOA WA KIKODI ARUSHA ILITEMBELEA KAMPUNI YA DOUBLE DIAMOND HOLDINGS LIMITED INAYOMILIKIWA NA BW. PARDEEP SINGH SIDHU ILIYOPO MKOA WA KIKODI WA ARUSHA MAENEO YA NJIRO
KAMPUNI HIYO INAJIHUSISHA NA UZALISHAJI WA POMBE KALI AINA YA THE ACE OF DIAMOND GIN NA THE ACE OF DIAMOND GIN PINEAPPLE
KATIKA UKAGUZI HUO ILABAINI KATONI 666 ZIKIWA ZIMEBANDIKWA STAMP ZINAZODHANIWA KUWA ZA KUGUSHI PAMOJA NA REEL MOJA YA STAMP INAZODHANIWA KUWA YA KUGUSHI.
SAMBAMBA NA HAYO TIMU MAALUM ILIBAINI KUWA KULIKUWA NA KATONI 995 ZIKIWA ZIMEZALISHWA MUDA MREFU LAKINI HAZIJA BANDIKWA STEMPU KINYUME NA UTARATIBU. TAYARI MTUHUMIWA AMEFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA USALAMA KWA HATUA ZAIDI.