Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Bw Fredrick Mtui (katikati) akitangaza kampeni mpya ambayo itamwezesha mteja wao kukopa fedha taslimu, fedha ya mkopo ya kununua umeme (LUKU) na fedha ya mkopo ya kununua muda wa maongezi. Kushoto ni Bi Sophia Mang’enya ambaye ni meneja masoko wa Taasisi ya Y9 na wa kwanza kulia ni afisa msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Bw Salim Bugufi. Kampeni hiyo pia itamwezesha mteja wao kushinda simu ya mkononi aina ya Samsung na pikipiki kila wiki kwa wiki nane wakati mshindi wa wiki ya tisa atashinda zawadi ya gari aina ya IST.
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Fredrick Mtui akitangaza kampeni mpya ambazo itamwezesha mteja wao kukopa fedha taslimu, kupata fedha za mkopo wa kununua umeme (LUKU) na fedha ya mkopo ya kununua muda wa maongezi.Kampeni hiyo pia itamwezesha mteja wao kushinda simu ya mkononi aina ya samsung na pikipiki kila wiki kwa wiki nane wakati mshindi wa wiki ya tisa atashinda zawadi ya gari aina ya IST.
Afisa Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Salim Bugufi akifafanua jambo wakati wa kutangaza kampeni mpya ya taasisi ya Y9 Microfinance ambayo itamwezesha mteja wao kukopa fedha taslimu, kupata fedha ya mkono wa kununua umeme (LUKU) na muda wa maongezi. Kampeni hiyo pia itamwezesha mteja wao kushinda simu ya mkononi aina ya samsung na pikipiki kila wiki kwa wiki nane wakati mshindi wa wiki ya tisa atashinda zawadi ya gari aina ya IST
………
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance, imezindua kampeni mpya yenye lengo la kumwezesha mteja wao kupata huduma tatu tofauti za kifedha.
Kupitia kampeni hiyo, wateja watapata mikopo nafuu ya fedha, malipo ya umeme (LUKU) na muda wa maongezi kwa kupitia teknolojia ya ubunifu ya hali ya juu na kisasa zaidi.
Lengo la kampeni hiyo ni kuwanufaisha wateja ambao wamewezesha taasisi hiyo kutimiza mwaka mmoja kwa mafanikio makubwa.
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance Bw Fredrick Mtui alisema kuwa kupitia teknolojia ya kisasa waliyowekeza, wateja wataweza kuwa na chaguo la kupata huduma bora na lengo la kufanya hivyo ni kuchochea maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwa pamoja na uchumi.
Mtui alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kutoa mikopo kwa haraka na unafuu zaidi yenye lengo la kukidhi mahitaji mbalimbali kama matumizi binafsi, kulipia deni la simu ya mkononi na malipo ya umeme.
Alisema kuwa wateja wao watapata fursa ya kuchagua kati ya mikopo hiyo mitatu kwa urahisi zaidi.
“Wateja wanaweza kupata msaada wa kifedha wanavyohitaji kwa haraka zaidi na unachotakiwa kufanya ni kupakua program au App ya Y9 Microfinance na kujiunga ili ufaidike na huduma hizi tatu,” alisema Bw Mtui.
Alisema kuwa taasisi ya Y9 Microfinance sio tu inatoa mikopo, bali inawezesha watu kufikia ndoto zao kwa kupitia ubinifu wa hali ya juu na wenye tija.
“Kupitia kampeni hii mpya, wateja wanapata fursa ya kuongeza kiwango cha mikopo na kuboresha hali ya kifedha. Kwa kukopa na kulipa mikopo kwa wakati, wateja atakuwa amejiboreshea nafasi zaidi ya kuongeza kiwango cha kukopa kuanzia sh2, 000 hadi sh100, 000,” alisema.
Aliongeza kuwa ili kuwanufaisha zaidi wateja wao, watachezesha droo kubwa wiki ya tisa ambapo mshindi atazawadiwa gari aina ya IST.
Mbali ya gari, pia kutakuwa na zawadi nyingine kama pikipiki na simu janja ya samsung.
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa michezo ya bodi ya kubahatisha nchini, Bw Salim Bugudfi aliipongeza taasisi hiyo kwa ubunifu wenye tija na kuwaomba Watanzania kuchangamkia fursa hiyo.