Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoani Pwani, imekuwa ya tatu kitaifa katika utoaji huduma kwa ufanisi kwa wateja wake.
Aidha mfuko huo umeahidi utendaji kazi unaoendana na kasi ya Nssf ya sasa ambayo inahitaji ujali kwa wateja na kutoa huduma bora.
Kaimu Meneja NSSF Pwani Rehema Mutungi akifunga maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kimkoa, alieleza utoaji huduma bora kwa wateja wao ni jadi yao na imeonyesha dhahiri nafasi waliyoipata kitaifa.
“Tunahitaji kufika namba moja ,huu ni utamaduni wetu kuhudumia wateja kwa ubora na kwa wakati ,tunaamini miaka ijayo tutafanya vizuri zaidi”alieleza Rehema.
Rehema anasisitiza ushirikiano,umoja kwa watumishi na watendaji wa NSSF ili kutoa huduma kwa ufanisi.
Vilevile Rehema alihimiza ,kila mmoja kujitathmini na kuchukua hatua za haraka kukabiliana na vitendo vya rushwa ili kudumisha imani kwa wanachama na wadau.
Katika kufunga maadhimisho hayo kimkoa wametoa vyeti na zawadi kwa waajiri watano pamoja na zawadi kwa mwanachama na wafanyakazi.
“Uwepo wa waajiri na wanachama ndio faraja yetu , safari hii tumetoa vyeti kwa waajiri watano ambao wamekidhi vigezo ikiwemo kulipa kwa wakati,kutokuwa na penati, mwakani tutatoa kwa idadi kubwa “
Nae mwajiri Patrick Semiono kutoka GFA vehicle assembler alishukuru kupata cheti,na kuongeza ni funzo kwao lakini wana uzoefu kwa kufanya kazi na sekta binafsi zaidi ya 18 sasa.
Semiono alieleza,kati ya sekta hizo 18 NSSF inatoa huduma nzuri ambapo hawamkeri mteja wao.
Kwa upande wa Mwanachama wa Nssf Kibaha, Vicent Ndumbili aliipongeza Nssf Mkoani hapo kwa kutoa huduma bora na kujali wateja.
Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ilianzishwa rasmi kimataifa mwaka 1984 kwa lengo la kutambua umuhimu wa huduma bora kwa wateja na juhudi za wafanyakazi wanaotoa huduma bora kwa wateja ambapo mwaka huu 2023 yalianza octoba 2-na octoba 6 imefikia kilele.