Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) hawapo pichani, wakati alipozindua bodi ya TAA jijini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) Juma Fimbo akifafannua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali Watu wa WIzara ya Uchukuzi Lucas Kambelenje akizungumza kwa Wajumbe, Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanywa na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mussa Mbura akifafanua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, wajumbe wa bodi, menejimenti na watumishi wa TAA (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akimmkabidhi vitendea kazi mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) Mhandisi Baraka Mwambage mara baada ya kuzindua bodi hiyo hawapo, jijini Dare es Salaam leo.
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa katika picha ya pamoja na wajuumbe wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) mara baada ua kuizindua, jijini Dar es Salaam leo.PICHA 7Baadhi ya Wajumbe wa Bodi Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipozindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo.
…….
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameitaka Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) kuhakikisha TAA inakuwa na vyanzo vingi vya Mapato ili kutoa huduma nzuri zaidi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati alipozindua rasmi bodi hiyo Waziri Prof. Mbarawa amesema uwepo wa vyanzo nje ya vile vinavyotozwa kupitia huduma za uendeshaji utaiwezesha TAA kuboresha viwanja vingi zaidi kwa muda mfupi.
“Kuna mapato mengi sana ambayo yanapatikana nje ya huduma za moja kwa moja zinazotolewa ndani ya Kiwanja, mkiweza kuja na mpango madhubuti kwenye eneo hilo TAA itafika mbali na itatimiza malengo yake kwa wakati’ amesema Waziri Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa ameitaka TAA kuhakikisha inapelekea watumishi wake kujifunza katika vya ndege mbalimbali duniani ili kuwaongezea ujuzi na utaalaam katika utendaji wa kazi.Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Juma Fimbo amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa watasimamia maeneo yote ikiwemo mifumo mipya iliyosimikwa viwanjani ili kutoa huduma za kisasa na viwango.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utalawa na Rasilimali Watu Lucas Kambelenje maewapongeza wajumbe wa bodi hiyo kwa kuteuliwa na kuwasisitiza kuzingatia miongozo.Bodi ya TAA iiliyozinduliwa inajumuisha wajumbe inaongozwa na Mwenyekiti Juma Fimbo, Mhandisi Baraka Mwambage, Meshack Anyingisye, John Njawa, Plasduce Mbosa na Biseko Chiganga.
(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Uchukuzi)