………………
Na Sixmund Begashe -Dodoma
Wizara ya Maliasili na Utalii imepongezwa kwa kazi nzuri ya usimamizi wa ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi awamu ya pili la Wizara hiyo lililopo Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma, ambalo lipo tayari kwa matumizi ya Shughuli za kiofisi.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, alipolitembelea Jengo hilo kwenye ziara yake na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi unaondelea kwenye mji huo wa kipeke nchini.
Aidha licha ya kuipongeza Wizara hiyo Dkt. Kusiluka amehimiza ukamikishwaji wa kazi chache zilizobaki kwenye ujenzi huo.
Akizungumzia ujenzi wa Jengo hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi ameleza kuwa hadi sasa ujenzi wa jengo hilo umeshafikia asilimia 99% na kuwa asilimia Moja iliyobaki ni ya kazi ndogo ndogo za mwisho.