Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo akizungumza katika kikao cha madiwani Ilala.
Madiwani wa Manispaa ya Ilala.
………………………..
Na Heri Shaban
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, ameagiza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji na Kamati zilizochaguliwa kuisaidia Serikali kukusanya Mapato katika kipindi cha robo ya tatu ili Halmashauri hiyo iweze kupata Mapato mengi na kuvuka lengo.
Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo, alitoa agizo hilo katika kikao cha Baraza la Madiwani la kumchagua Naibu Meya wa jiji hilo Ojambi Masaburi aliyeshinda kwa kishindo kwa kupata kura zote 45 ambapo sasa hivi Masaburi anashika nafasi hiyo kwa kipindi cha awamu ya pili.
“Nawapongeza Madiwani na Baraza la Halmashauri kwa ujumla kwa umoja wao na ushirikiano pamoja na viongozi wa chama cha Mapunduzi CCM kwa malezi mazuri naomba sasa mshirikiane kuisaidia Serikali kukusanya Mapato “alisema Mpogolo.
Mkuu wa Wilaya Mpogolo aliwapongeza viongozi na wajumbe kwaukomavu wao sasa hivi wamerudi katika baraza wawe wamoja katika utekelezaji wa majukumu yao ambapo walichokifanya leo ndio watafanya mwaka 2024 katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ajili ya kushika dola.
Alitoa agizo waliochaguliwa wamsaidie Mkurugenzi Jomary Mrisho Satury, katika kushika dola pamoja na kuisaidia Halmashauri kukusanya Mapato kwani baraza hilo na kamati zake wanawajibu wa kuisaidia Serikali na kumsaidia Meya Omary Kumbilamoto na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Aliwataka wawe wasimamizi wakuu wa miradi ya Serikali ikiwemo kufanya ziara katika miradi ya sekta ya Elimu kutatua changamoto mbali mbali.
Aidha aliwagiza Madiwani waliochaguliwa wafanye kazi kwa weledi na kushirikiana na Mkurugenzi wa jiji hilo ambapo amekuwa mbunifu katika ufanyaji kazi zake na kusimamia mapato vizuri.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapunduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde alisema CCM itatoa ushirikiano kwa baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo iweze kutekeleza majukumu yake na chama hicho kitawaita kwa ajili ya semina mbali mbali kwa ajili kujiandaa na Serikali za mitaa.
Mwenyekiti Sidde aliwataka madiwani wa Ilala kujenga umoja na kushirikiana na kuakikisha chama kinashinda katika chaguzi zake za kusaka dola na kuwataka kila Diwani kufanya mikutano ya kila kata kueleza utekelezaji wa Ilani unaofanywa na Serikali.
Meya wa jiji Omary Kumbilamoto aliwataka madiwani wake kuakikisha wanatoa ushirikiano kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Jomary Mrisho Satury katika ukunyaji Mapato ya Serikali na kusimamia miradi ya maendeleo ndani ya Halmashauri hiyo.
Aidha Meya Kumbilamoto aliwapongeza Wenyeviti wa Kamati wote waliochaguliwa katika uchaguzi huo pamoja na Naibu Meya Ojambi Masaburi aliyeshinda nafasi hiyo awamu ya pili mfululizo.
Akizungumza katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Jomary Mrisho Satury alisema katika kipindi cha robo quater Halmashauri hiyo imeweza kukusanya shilingi bilioni 25 sawa na asilimia 100 ya Mapato kutokana na kadi mbali mbali.
“Ushirikiano wa watendaji wangu katika kipindi cha miezi mitatu tumeweza kukusanya Mapato kwa asilimia 100 makusanyo makubwa ni Ushirikiano na madiwani wake wa Halmashauri hiyo “alisema Satury.
Mkurugenzi Jomary Mrisho Satury alisema katika kipindi hicho cha robo ya mwaka Mapato wamefanya vizuri na mikakati yao waliojiwekea kuvunga lengo wakusanye zaidi ya asilimia 100.
Mkurugenzi Jomary aliwashukuru Madiwani na Kamati za Kudumu waliomaliza muda kwa kufanya kazi vizuri na kutoa ushirikiano katika ukusanyaji Mapato.