MISS Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu (kushoto) akimpongeza Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Jokate Mwegelo, wakati wa hafla ya kumpongeza iliyoandaliwa na umoja huo Dar es Salaam, octoba 4.Jokate pia alishika nafasi ya pili katika Shindano la Miss Tanzania mwaka 2006.
………………………
Na Sophia Kingimali
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Taifa(UWT) Joketi Mwegelo amewataka wanawake kuishi kwa kupendana na kusaidiana ili kuendelea kusapoti juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwainua wanawake.
Hayo ameyasema Oktona 4, 2023 jijini Dar es salaam wakati alipofika kuchukua barua yake ya uteuzi ofisi za CCM mkoa ambapo alilakiwa na viongozi mbalimbali wa UWT.
Amesema Rais Dkt. Samia amewaheshimisha wanawake duniani kote hivyo hawanabudi kumuunga mkono kwenye juhudi zake za kuhakikisha nchi inasonga mbele.
“Wanawake tunapaswa kuishi kwa kupendana,kuheshimiana na kusaidiana ili kuhakikisha tunafika mbali kwani wanawake ni jeshi kubwa”amesema Mwegelo.
Aidha amewataka UWT kushirikiana nae katika kusukuma maendeleo kwani ameingia kwenye jumuiya ambayo imejipanga.
“Hii nafasi niliyopata ni ya UWT wote tunapaswa kushirikiana vyema ili kuhakikisha wanawake wote nchini tumuunge mkono Rais wetu ambaye anazidi kuifungua nchi yetu”
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT Dar es salaam Mwajabu Mbwambo amesema umoja huo umepata kiongozi ambaye ni shupavu hivyo wanaimani atafikisha umoja huo mbali na kutatua changamoto zilizopo.
Nao wasanii waliofika kumsindikiza katibu mkuu huyo wamempongeza Rais kwa kumuamini Joketi Mwegelo hivyo ni matumaini yao atafikisha jumuiya hiyo mbali.
Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake Msanii Wema Issack Sepetu amesema kuteuliwa kwa katibu huyo ni imani ya Rais kwa vijana hivyo wanapaswa kutumia fursa hiyo vizuri.
Mapokezi rasmi ya kumpokea katibu mkuu huyo wa UWT yanatarajiwa kufanyika jijini Dodoma Oktoba 17,2023 na ameahidi baada ya kukabidhiwa ofisi ataongea kuhusu muelekeo wa UWT.