Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Equity Bi. Isabella Maganga akizungumza kuhusu huduma ya Kidigital ya Live Chat katika Kituo Cha huduma kwa Wateja ambayo inatoa fursa kwa wateja kuwa karibu na watoa huduma pamoja na kufanya mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya saa 24 wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye tawi la benki hiyo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Equity Bi. Isabella Maganga akisisitiza jambo wakati akizungumza kuhusu huduma ya Kidigital ya Live Chat katika Kituo Cha huduma kwa Wateja ambayo inatoa fursa kwa wateja kuwa karibu na watoa huduma pamoja na kufanya mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya saa 24 wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye tawi la benki hiyo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Magreth Makundi Meneja wa Tawi la Mwenge Benki ya Equity, akifafanua baadhi ya mambo katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye tawi la benki hiyo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Equity Bi. Isabella Maganga kulia akiwasiliana na wateja kwa kutumia huduma ya Kidigital ya Live Chat katika Kituo Cha huduma kwa Wateja ambayo inatoa fursa kwa wateja kuwa karibu na watoa huduma pamoja na kufanya mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya saa 24 wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye tawi la benki hiyo Mwenge jijini Dar es Salaam. kushoto ni Magreth Makundi Meneja wa Tawi la Mwenge Benki ya Equity.
Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Equity Bi. Isabella Maganga kulia akzindua huduma ya Kidigital ya Live Chat katika Kituo Cha huduma kwa Wateja ambayo inatoa fursa wateja kuwa karibu na watoa huduma pamoja na kufanya mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya saa 24 wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye tawi la benki hiyo Mwenge jijini Dar es Salaam.
NA JONH BUKUKU, DAR ES SALAAM
Benki ya Equity imezindua huduma ya Kidigital ya Live Chat katika Kituo Cha huduma kwa Wateja ambayo inatoa fursa kwa wateja kuwa karibu na watoa huduma pamoja na kufanya mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya saa 24.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 4, 2023 Jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Equity Bi. Isabella Maganga, amesema kuwa katika kuanzimisha wiki ya huduma kwa wateja wamezindua huduma ya Light Chat ili kuwafikia wateja na kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora na rafiki.
“Huduma hii inakwenda kutuweka karibu na wateja wetu ambapo mteja na mtoa huduma wanaongea moja kwa moja live kutoa huduma papo kwa papo” amesema Bi. Maganga.
Bi. Maganga amesema kuwa kazi yao kubwa ni kutoa huduma ya fedha na kuendelea kujituma na kubuni huduma zao, huku akieleza kuwa watahakikisha wateja wao wanaendelea kufurahia huduma zao za kibenki.
Aidha amewashukuru wateja kwa kusherekea pamoja katika muda wote wa wiki ya huduma kwa wateja, huku akiahidi kuendelea kufanya vizuri katika sekta ya Benki.
Naye Magreth Makundi Meneja wa Tawi la Mwenge Benki ya Equity, amesema kuwa watahakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa kiwango vya juu.
Amesema kuwa huduma ya Kidigital ya Live Chat inakwenda kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao hasa kuwa karibu na wateja wao katika kutoa huduma.