Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Kitaifa Bw. Abdallah Shaibu Kaim akipanda mti katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma leo Oktoba 3, 2023 katika eneo la mradi wa Hifadhi ya Mazingira kupitia upandaji wa miti ambapo jumla ya miti 146 imepandwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Kitaifa Bw. Abdallah Shaibu Kaim akizungumza wakati wa zoezi la upandaji wa miti na ukaguzi wa miradi katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma leo Oktoba 3, 2023 katika eneo la mradi wa Hifadhi ya Mazingira kupitia upandaji wa miti ambapo jumla ya miti 146 imepandwa.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Alhaj Jabir Shekimweri akipanda mti katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma leo Oktoba 3, 2023 katika eneo la mradi wa hifadhi ya mazingira kupitia upandaji wa miti ambapo jumla ya miti 146 imepandwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bw. John Kayombo akimwagilia mti alioupanda wakati wa Mwenge wa Uhuru 2023 ukikagua miradi ya maendeleo katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma Oktoba 3, 2023 katika eneo la mradi wa hifadhi ya mazingira kupitia upandaji wa miti ambapo jumla ya miti 146 imepandwa.(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).
………
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Kitaifa Bw. Abdallah Shaibu Kaim amesema ameridhishwa na utunzaji wa uhifadhi wa mazingira unaotekelezwa na wananchi katika maeneo mbalimbali.Amesema hayo wakati akipandaji mti na kukagua miradi ya maendeleo katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) ambapo jumla ya miti 146 imepandwa kati yake miti aina ya miashoki ni 129 na 15 aina ya jakalanda.
“Mwenge wa Uhuru mwaka huu una lengo la kuelimisha na kuhamasisha Watanzania juu ya athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi ambazo kimsingi asilimia 95 zinasababishwa na shughuli na matendo ya kibinadamu zinazofanywa katika Maisha yetu ya kila siku.
“Moja wapo ikiwa ni ukataji miti kiholela hivyo tuepuke kufanya hivyo bali tushirikiane katika upandaji wa miti, mambo mengine yasiyofaa ni uchomaji moto misiti, kilimo na ufugaji karibu na vyanzo vya maji naomba tufanye shughuli zetu umbali wa mita 60 kutoka vyanzo vya maji,” amesema Kaim.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa utupaji taka kiholela, uchimbaji wa madini usiozingatia uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na ufugaji wa kuhamahama nao uchangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa mazingira.
Amebainisha kuwa athari mojawapo ya mabadiliko ya tabianchi zinazotokana na uharibifu wa mazingira ni pamoja na ukame, mafuriko, upoteaji rotuba, kukosa mvua na kuongezeka kwa joto sambamba na mabadiliko ya msimu wa mvua na mwisho kukosa chakula na kuathiri uchumi wa nchi.
Kaim amesema upandaji miti unakwenda kutekeleza agizo la Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan yenye lengo la kuhakikisha kila mtanzania anashiriki katika uhifadhi wa mazingira ikiwa hatua ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Kwa upande wa Waziri wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Mhe. Anthony Mavunde amesema wataendelea kuenzi na kusimamia kaulimbiu ya Serikali ya kuhakikisha wanatunza mazingira ili yalete manufaa.
Mhe. Mavunde amesema ili kufikia lengo hilo wataendelea na kampeni mbalimbali za kuhakikisha mazingira yanatunzwa ili kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
“Kwa kutambua kuna changamoto ya ukataji wa miti hivyo tumeandaa programu maalumu ambayo tutawezesha wananchi wetu kuacha kukata miti kwaajili ya kutengeneza mkaa na baladala yake tutawahimiza kuanza kutengeneza mkaa kwa kutumia makaratasi na uchafu ambayo itasaidia kutunza mazingira,” amesisitiza.
Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu 2023 unaohusu Mabadiliko ya Tabianchi Hifadhi Mazingira sambamba na Utunzaji wa Vyanzo vya Maji “Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa.”