Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo Amewasili Mkoani Katavi tayari kuanza ziara yake ya kikazi itakayoanza leo tarehe 03/10/2023.
Pamoja na Mambo mengine Chongolo amemwagiza waziri wa nishati na naibu waziri mkuu Mhe.Dk.Dotto Biteko kuhakikisha anatafuta njia za haraka za kumaliza tatizo la umeme mkoani Katavi ili kuongeza kasi ya shughuli za maendeleo.
Aidha Chongolo amewataka baadhi ya wananchi wa Mkoa huo kuachana na imani zinazoweza kurudisha nyuma maendeleo badala yake wajikite katika fikra za mafanikio kwani Katavi ni moja ya Mikoa iliyotoa mchango mkubwa kwa Nchi ikiwepo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.
Katibu Mkuu Chongolo na ujumbe wake watatembelea Wilaya zote za mkoa wa Katavi ili kukagua uhai wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM ikiwepo kukagua miradi ya Maendeleo.