Baada ya kufikia lengo la makusanyo katika mapato ya mwezi septemba ,Timu ya Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Njombe imecheza mechi ya shukrani kwa mlipa kodi dhidi ya wafanyabiashara FC katika Dimba la Sabasaba mjini Njombe na kisha kupoteza kwa kichapo cha bao 3-0.
Mbali na kutoa shukrani kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Njombe kwa kutoa ushirikiano na uzalendo wa dhati kwa mamlaka ya mapato,Mchezo huo wa mpira wa miguu uliyochagizwa na kampeni ya mashine za EFD ya TUWAJIBIKE umelenga kuwasogeza jirani na kuongeza udugu baina ya pande hizo mbili
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao umewafanya wafanyabiashara kutoka kifua mbele kwa ushindi wa bao tatu kwa sifuri ,nikazungumza na meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Njombe Spesioza Owure na mwenyekiti wa wafanyabiashara mji wa Njombe Eliud Mgeni Pangamawe ambao wanasema kuletwa kwa mchezo huo kunafungua mashirikiano kati ya maofisa wa TRA na wafanyabiashara .
Kwa upande wao wao wachezaji akiwemo Joseph Makweta maarufu kichuya kapteni wa timu ya wafanyabiara anasema wapinzani wao walizidiwa kwenye kungo huku kapteni wa TRA fc akisema walikosa mazoezi hivyo wanakwenda kujipanga kwa marudiano.
Wakati mamlaka ya mapato ikicheza mechi ya shukrani,katika Uwanja wa Matembwe halmashauri ya wilaya ya Njombe nayo imefanya bonanza la afya ambalo limehusisha michezo na upimaji wa magonjwa mbalimbali kama ambavyo Christopher Sanga mkurugenzi Njombe DC ambaye anasema bonanza hilo linakwenda kutoa fursa ya kupima maradhi bure.