Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza kwenye hafla ya chakula cha hisani iliyoandaliwa kwa ajili ya kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa jumla wa Kanisa Katoliki la Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimkabidhi Sh.10 milioni kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango kwenye hafla ya chakula cha hisani iliyoandaliwa kwa ajili ya kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa jumla wa Kanisa Katoliki la Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Askofu Msaidizi Vicent Mpwaji akizungumza kabala ya kumkribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na waalikwa kwenye hafla ya chakula cha hisani iliyoandaliwa kwa ajili ya kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa jumla wa Kanisa Katoliki la Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa na baadhi ya Mapdri wakti akitembezwa katika Kanisa Katoliki la Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni jijini Dar es Salaamkabala ya hafla ya chakula cha hisani iliyoandaliwa kwa ajili ya kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa jumla wa kanisa hilo
Baadhi ya Masista wa Kanisa Katoliki la Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza kwenye hafla ya chakula cha hisani iliyoandaliwa kwa ajili ya kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa jumla wa Kanisa hilo
…………..
Na. Lusungu Helela-DSM
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inathamini na kutambua mchango mkubwa wa taasisi za dini katika shughuli mbalimbali za maendeleo hususani katika kuimarisha amani na utulivu wa nchi.
Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango kwenye hafla ya chakula cha hisani iliyoandaliwa kwa ajili ya kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa jumla wa Kanisa Katoliki la Parokia ya Utatu Mtakatifu Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Simbachawene amewapongeza wanaparokia hao kwa hatua kubwa waliyofikia katika ujenzi wa kanisa hilo huku akiwasihi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika masuala ya maendeleo.
“Hongereni sana kwa hatua hii kubwa mliyofikia ya umaliziaji wa Kanisa hili, hakika mmefanya kazi kubwa na nzuri” amesema Mhe.Simbachawene.
Aidha, Mhe. Simbachawene amewapongeza wanaparokia hao kwa kuwa na mpango kazi makini wa ukamilishaji wa kanisa hilo ambapo wanatarajia ifikapo tarehe 7 Januari, 2024 litatabarukiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Thaddeus Ruwa’ichi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Parokia ya Kanisa hilo, Gallen Mvungi jumla ya kiasi cha shilingi milioni 250 kinahitajika kukamilisha ujenzi wote ambapo shilingi milioni 50 tayari zimeshakusanywa na wanaparokia hiyo.
Katika hafla hiyo, jumla ya kiasi cha shilingi milioni 110 zilikusanywa huku kiasi cha shilingi milioni 78 zikiwa ni ahadi na shilingi milioni 32, fedha taslimu.
Hafla hiyo ilitanguliwa na misa maalum ilyoongozwa na Mwakilishi wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Askofu Msaidizi Vicent Mpwaji na kuhudhuriwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Bw. Masanja Kadogosa.