Na Joachim Nyambo, Chunya.
MBUNGE wa Jimbo la Lupa wilayani Chunya Mkoani Mbeya, Masache Njelu Kasaka ametoa mchango wa Shilingi Milioni moja kwaajili ya kusaidia uendelezaji wa miradi mbalimbali ya Kanisa la Moravian Ushirika wa Chunya.
Masache ametoa mchango huo aliposhiriki Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Moravian Ushirika wa Chunya ambapo pamoja na kushiriki Ibada takatifu, Mbunge huyo pia alipata nafasi ya kuwasalimu waumini walioshiriki Ibada hiyo.
Katika salamu zake Masache amewaomba waumini wazidi kuliombea Taifa liwe na Amani ili Serikali izidi kuleta Maendeleo kwa wananchi..