Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Hashim Komba akizungumza na wananchi na wadau mbalimbali ambao wamejitokeza katika zoezi la ufanyaji wa usafi wa Jumamosi ya mwisho wa Mwezi ambao umefanyika mapema leo katika kata ya Makurumla Kwenye Wilaya hiyo.Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Hashim Komba akiwa sambamba na Afisa Mazingira anayeshughulikia Udhibiti wa takangumu na Usafirishaji Manispaa ya Ubungo Lawi Bernad katika zoezi la ufanyaji wa usafi wa Jumamosi ya mwisho wa Mwezi ambao umefanyika mapema Leo katika kata ya Makurumla Kwenye Wilaya hiyo.
Afisa Mazingira anayeshughulikia Udhibiti wa takangumu na Usafirishaji Manispaa ya Ubungo Lawi Bernad akizungumza na mabalozi wa Mazingira Osca Richar ambaye nj Bondia wa Ngumi za kulipwa,Mr Abdul Latwif Maundu Pamoja na lulu Sadru Sengulo wakati waliposhiriki zoezi la ufanyaji wa usafi leo katika kata ya Makurumla Kwenye Wilaya hiyo.
Baadhi ya wananchi na wadaubalimbali ambao wamejitokeza katika zoezi la ufanyaji wa usafi wa Jumamosi ya mwisho wa Mwezi ambao umefanyika mapema ambao ulianzia Kata ya Makurumla eneo la Mwembechai hadi Kagera kwenye Wilaya hiyo.
……………………
NA MUSSA KHALID
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Hashim Komba amewataka wananchi wa kushiriki kimamilifu katika Usafishaji wa mito na mitaro ya maji katika maeneo yao ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza ya kiafaya hasa katika kipindi Cha mvua zinazotarajiwa kunyeesha.
Mkuu Huyo wa wilaya ameeleza hayo mapema leo jijini Dar es salaam wakati aliposhiriki katika zoezi la ufanyaji wa usafi na wananchi wa Ubungo mtaa wa sisi kwa sisi katika kata ya Makurumla ambapo ni muendelezo wa kampeni ya kuisafisha na kuipendezesha Ubungo lakini pia lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya taarifa iliyotolewa na Mamlaka kuhusu kunyeesha mvua kubwa ya EL NIÑO.
Amewasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari Kila Mmoja Kwa nafasi yake kuhakikisha wanasafisha Mazingira yao kila wakati Ili kuepukana na madhara.
“Leo tunafanya usafi Kwenye mto huu maana yake wanaotupa taka ni sisi wenyewe,wanaoziba njia za maji na kupata mafuriko ni sisi wenyewe hivyo kupanga ni kuchagua tusisubiri malalamiko Bali tuwadhibiti wanaotupataka hovyo Kwenye mito”amesema DC Komba
Aidha ametoa rai mwa Mkurugenzi kuhakikisha anasisimamia kikamilifu usafishaji wa mito Gide,na China Kwa haraka ili kuacha njia ya maji ipitike.
Kwa upande wake Afisa Mazingira anayeshughulikia Udhibiti wa takangumu na Usafirishaji Manispaa ya Ubungo Lawi Bernad amesema zoezi hilo la ufanyaji wa usafi ni la muendelezo hivyo Leo wamesafidha mitaro na njia zinazopotisha maji ikiwa ni tahadhari ya kukabiliana na mvua.
“Sisi Tar 26 tulizindua kampeni ya ‘kataa uchafu safisa pendezesha Ubungo” maeneo ya Mazese ambapo ni lazima kila mwananchi afikiwe na awe na uelewa wa kuwa mdau wa usafishaji wa Mazingira kwani ni endelevu na katika mitaa yote 90 ya Halmashauri ya Masipaabya Ubungo ambapo pia tutakuwa tunatoka zawadi kwa mitaa ambayo inasafisha Ubungo na kuipendezesha ambapo mshindi wa kwanza atapewa laki sita,wa pili laki tatu na mshindi wa tatu atapewa laki moja”amesema Lawi
Amewasisitiza wananchi kuondoa dhana ya kuwa ufanyaji wa usafi ni mpaka serikali pekee bali wafanye usafi kwani Maisha ni yakwao na Wilaya ikiwa safi Maisha yao yatakuwa ni bora zaidi.
Naye Diwani wa Kata ya Makurumla Bakari Kimwanga amewataka wananchi kuendelea kushirikiana katika ufanyaji wa usafi Kwenye maeneo yao kwani itasaidia Jamii kuweza kustaharabika.
Amesema kuwa malengo yao ni kuhakikisha wanadumisha ufanyaji wa usafi ili waweze kuibuka vinara kuwa kata iliyosafi zaidi.
Mabalozi wa mazingira Wilaya ya Ubungo akiwemo Osca Richar ambaye nj Bondia wa Ngumi za kulipwa,Mr Abdul Latwif Maundu Pamoja na lulu Sadru Sengulo wamesema kuwa wataendelwa kuwa beba Kwa bega na Manispaa ya Ubungo ikiwemo kutoa elimu kwa jamii namna ya kuiisafidha na kuipendezesha Ubungo Ili Wilaya hiyo iendelee kuwa Bora ya Usafi wa Mazingira nchini.
Wadau mbalimba wameshiriki katika zoezi hilo la usafi ambalo limefanyika kata ya Makurumla wakiwemo Viongozi wa kisiasa,Taasisi na mashirika mbalimbali.