Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imeibuka kidedea kwa kuwa Mshindi wa Pili wa Jumla katika Maonesho ya 6 ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika Mkoa wa Geita,
Tuzo hiyo imetolewa Leo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman katika uwanjani wa Bomba mbili Geita.
Ushindi huo unatokana na ubunifu Makini kwa kuleta Nishati mbadala ya kupikia kwania ya kuwatua kuni kichwani akina Mama na kushirikiana na makundi maalum kwa kuwasaidia kiuchumi na kiteknolojia Kama watu wenye ulbino na viziwi.
Pia STAMICO walishirikiana na kikundi cha Wanawake na Samia Mkoa Geita kwa kuwapa uwakala wakuuza nishati mbadala ya kupikia ili kukuza uchumi wao na kuwaelimisha wanawake wenzae juu ya matumizi sahihi ya nishati hiyo ya Rafiki briquettes.
Ikumbukwe kuwa hii ni zaidi ya mara tatu mfululizo kwa STAMICO kupata ushindi tangu kuanza kwa maonesho hayo ya madini .