Afisa uhusiano Mwandamizi TASAC Amina Miruko akizungumza na waandishi wa habari katika banda la shirika hilo kwenye maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita kulia ni Victoria Myonga Afisa Udhibiti Huduma za Bandari TASAC.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kalvin akizunguma na waandishi wa habari katika banda la shirika hilo kwenye maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita kulia ni Victoria Myonga Afisa Udhibiti Huduma za Bandari TASAC.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kalvin akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde wakati alipotembelea katika banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwenye maonesho ya Teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita, Katikati ni Afisa uhusiano Mwandamizi TASAC Amina Miruko.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kalvin akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde wakati alipotembelea katika banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwenye maonesho ya Teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita, Katikati ni Afisa uhusiano Mwandamizi TASAC Amina Miruko na kushoto ni Victoria Myonga Afisa Udhibiti Huduma za Bandari TASAC
Wafanyakazi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakiwa katika picha ya pamoja katika banda la shirika hilo kwenye maonesho ya Teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita.
Na Mwandishi Wetu, Geita
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limewataka wachimbaji kuhakikisha wanazingatia kanuni za usalama wa usafiri wa majini kwa kutumia bandari rasmi.
Akizungumza leo Septemba 29,2023 na waandishi wa habari katika Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Tasac, Martha Kelvin, amesema wanashiriki maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu shughuli mbalimbali wanazofanya.
“Tasac ilianzishwa ili kudhibiti na kusimamia sekta ya majini kama vile bahari, maziwa, mabwawa na mito. Wachimbaji pia wanatumia usafiri wa majini kwa kusafiri ama kusafirisha bidhaa zao ndio maana katika maonesho haya tunatoa elimu ya masuala mbalimbali ya usafiri majini,” amesema Martha.
Naye Ofisa Udhibiti wa Huduma za Bandari Tasac, Victoria Miyonga, amesema ili kuhakikisha usalama wa usafiri wa majini kabla chombo hakijasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine ni lazima kikaguliwe.
“Tunajiridhisha kwa kupata taarifa kamili ya chombo husika, huwa tuna utaratibu maalumu kabla chombo hakijaondoka tunapata taarifa za kila chombo kinachosafiri.
“Tunahakikisha tunajua idadi ya abiria wanaosafiri, kiasi cha mzigo unaosafirishwa na kuna wenzetu tunaofanya nao kazi wanahakikisha chombo kinachotumika kimesajiliwa na kinatambulika rasmi na wanaokiendesha wana utaalam wa kutosha…tunawashauri wananchi wahakikishe wanatumia bandari rasmi kabla ya kuanza safari zao,” amesema Miyonga.
Ofisa huyo amesema wanashughulika na mnyororo mzima wa usafirishaji kuanzia anayesafirisha, anayehakiki mzigo kwenye shehena, mwenye meli, bandari husika inayopokea mzigo na unakokwenda kuhifadhiwa.
Amesema pia wanadhibiti huduma za bandari na usafiri wa njia ya maji ambapo kuna mawakala wa forodha, meli, wakusanyaji na watawanyaji wa mizigo, wahakiki shehena.
“Tunadhibiti wale wanaopima mizigo inayosafirishwa nje ya nchi, wanaofanya huduma ndogondogo bandarini, tunawadhibiti waendesha bandari kavu. Huwa tunatoa leseni kwa watoa huduma na kuhuhisha au kufuta,” amesema.
Kwa upande wake Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Tasac, Amina Miruko, amesema wanafanya kaguzi mbalimbali kuhakikisha wanaoviendesha vyombo wanakuwa na utaalamu wa kutosha.
“Tunahakikisha kunakuwa na vyombo vya usalama ili inapotokea tatizo au dharura yoyote abiria waokolewe na kutoka salama,” amesema Miruko.