Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania – TPA imetakiwa kuimarisha huduma zake na kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika kutanua masoko yake ili kuwafikia Wateja wa ndani na wa Kimataifa.
Wito huo umetolewa tarehe 29 Septemba, 2023 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara alipotembelea Banda la TPA katika maonesho ya sita ya teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya EPZA Bombambili Mjini Geita.