Waziri wa habari mawasilino na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akiUngumza katika mkutano wa Jukwaa la Uhuru wa mtandaoni Barani Afrika jijini Dar ea Salaam.
………………………….
Na Sophia Kingimali
Waziri wa habari mawasilino na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye amesema nchi itaendelea kuwa waumini wa uhuru wa mtandaoni huku akitoa rai kuwa uhuru huo unapaswa utumike kulinda tamaduni za nchi.
Hayo ameyasema leo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la uhuru wa mitandao barani Afrika linalofanyika jijini Dar es salaam.
Amesema pamoja na nchi kutoa uhuru wananchi wanapaswa kulinda tamaduni kwa kutumia mitandao hiyo katika shughuli za kuwaingizia kipato na si kutumia katika mambo ambayo yanaweza kuvunja amani ya nchi na kuchafua utu wa mtu.
“Tumeweka katika sera zetu uhuru wa mitandao lakini sasa hivi Dunia imekua tumieni mitandao hiyo kufanya shughuli za kiuchumi na si kupiga umbea ambao haukusaidii chochote”amesema Nape.
Amesema pamoja na kuwa na uhuru mtandaoni nchi za Afrika zinapaswa kulinda tamaduni na ili kuepusha nchi hizo kuingia kwenye matatizo ambayo yatapelekea kuharaibu amani na kuleta machafuko.
“Tusiondoke kwenye mtandao kila mtu ajiunge huko lakini tuhakikishe tunabaki salama kwa maslahi ya nchi zetu”
Sambamba na hayo Nape amesema kuwa nchi inajipanga chaguzi zijazo ziweze kutumia teknolojia kwenye uchaguzi ili kumuezesha kila mtu kuchagua viongozi popote atakapokua.
“Tunataka ifike mahali kila mwananchi awe na uwezo wa kupiga kura mtandaoni kusiwe na haja ya kwenda kwenye vituo na kupanga foleni kama kila mtu anaweza kutumia simu basi inawezekana ni sisi kuamua kwa kuweka sera nzuri na utekelezaji”ameongeza Nape
Kwa upande mbunge wa viti maalum Neema Rungangila amesema kuwepo kwa mkutano huu nchini kumetokana na juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua nchi kimataifa na kuimarisha uhuru wa habari,uhuru wa kujieleza na haki za binadamu