Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde akifungua semina kuhusu fursa zilizoko katika mnyororo wa thamani kwenye sekta ya Madini hasa watoa huduma katika migodi, Semina hiyo inafanyika ukumbi wa Mkapa kwenye maonesho ya teknolinia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita.
Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde akipiga makofu pamoja na Mbunge wa Geita mjini Mh. Constantine Kanyasu wakati wa semina kuhusu fursa zilizoko katika mnyororo wa thamani kwenye sekta ya Madini hasa watoa huduma katika migodi, Semina hiyo inafanyika ukumbi wa Mkapa kwenye maonesho ya teknolinia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO Dkt. Venance Mwase akifuatilia kwa makini wakati wa ufunguzi wa semina kuhusu fursa zilizoko katika mnyororo wa thamani kwenye sekta ya Madini hasa watoa huduma katika migodi, Semina hiyo inafanyika ukumbi wa Mkapa kwenye maonesho ya teknolinia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita.
Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Wanawake na Samia cha Mkoani Geita kinachofadhiliwa na STAMICO wakifuatilia hotuba ya waziri wa madini Mh. Anthony Mavunde wakati alipokuwa akifungua semina hiyo.
Baadhi ya viongozi wa kikundi cha watu wenye ulemavu wa ngozi kinachofadhiliwa na STAMICO wakifuatilia hotuba wakati wa ufunguzi wa semina hiyo mjini Geita.
Meneja wa Masoko na Mawasiliano Shirika la Madini la Taifa STAMICO Bw. Geofrey Meena akifuatilia hotuba ya Waziri wa madini wakati alipokuwa akifungua semina hiyo katika maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita.
…………………………………
NA JOHN BUKUKU, GEITA
Serikali kupitia Wizara ya Madini imejipanga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ikiwemo kuchochea, kufanikisha shughuli za madini pamoja na kuongeza wigo wenye kuleta tija kwa Taifa.
Akizungumza leo Septemba 28, 2023 wakati akifungua semina kuhusu fursa zilizopo katika mnyororo wa thamani kwenye sekta ya Madini hasa watoa huduma katika migodi, iliyofanyika Ukumbi wa Mkapa kwenye Maonesho ya Teknolojia ya Madini, Viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, amesema kuwa ni vizuri kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujenga uchumi na kuhakikisha kila mtanzania ananufaika.
Mhe. Mavunde amesema kuwa kupitia sera, sheria, miongozo serikali imerahisha shughuli za madini ili kuleta maendeleo.
“Uendeshaji wa migodi unaitaji zaidi uwezo na mafunzo jambo ambalo litasaidia kuendelea kutekeleza majukumu kwa uweledi” amesema
Mhe. Mavunde.
Ameeleza kuwa wakati umefika kwa sekta binafsi kuongeza nguvu katika uzalishaji wa bidhaa bora ili kuleta matokeo chanya katika sekta ya madini.
Mhe. Mavunde ameipongeza Serikali ya Rais Dkt. Samia Suruhu Hassan kwa kutengeneza mazingira rafiki na wezeshe kwa kufanya uwekezaji na kuchangia kwa asilimia kubwa kukuza kwa sekta ya madini.
“Tume ya madini imekuwa ikifanya kazi vizuri na kuleta maendeleo katika sekta hii muhimu” amesema Mhe. Mavunde.
Katika semina hiyo wadau katika sekta ya madini watapata fursa zilizopo katika mnyororo wa thamani hasa watoa huduma katika migodi pamoja na kujadili kwa pamoja namna sekta ya madini inavyoweza kutoa mchango kwa maendeleo ya Taifa.