Tayari tumeshazoea utamaduni wetu ambao pale YANGA inapofanya vizuri tunatamani kuiona SIMBA inafanya vibaya.
Furaha ya YANGA inakuwa si ya kutosha sana kwa sababu mpinzani wake bado ameimarika .
Tunakumbuka wakati SIMBA inafanya vizuri miaka minne 4 mfululizo YANGA walikuwa wapo hoi.
Kinachowasugua YANGA wanafanya vizuri kipindi ambacho mpinzani wao pia bado yupo imara.
Kipindi SIMBA inacheza robo fainali CAF YANGA ilikuwa hata hatua ya makundi kwao ni shida.
Lakini kwa sasa YANGA imeimarika bado wapinzani wao hatua ya makundi kwao kitu cha kawaida sana.
Kinacholazimishwa kwa namna yeyote ile mmoja anapofanya vizuri basi mmoja awe mbovu .
Na ndio maana hata wachambuzi tumeingia kwenye mtego wa kulazimisha SIMBA iwe mbovu wakati takwimu zinatusuta.
MANENO KUTOKA KWA MWANASOKA WA ZAMANI AMRI KIEMBA