Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD), Bw. Mavere Tukai akizungumza jambo katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambao umefanyika leo Septemba 27, 2023, katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JINCC), Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deogratius Balile akizungumza jambo katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambao umefanyika leo Septemba 27, 2023, katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JINCC), Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Daudi Kosuna akizungumza katika mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari na Bohari Kuu ya Dawa Tanzania ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambao umefanyika tarehe 25 Septemba 2023, katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JINCC), Dar es Salaam.
Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari Kuu ya Dawa Tanzania ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambao umefanyika tarehe 25 Septemba 2023, katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JINCC), Dar es Salaam.
……
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD) imefanikiwa kupiga hatua katika sekta ya afya baada ya upatikanaji wa bidhaa za afya kuongezeka kutoka asilimia 51 kwa mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 64 kwa mwaka 2023.
Akizungumza katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambao umefanyika leo Septemba 27, 2023, katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JINCC), Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD), Bw. Mavere Tukai amesema kuwa upatikanaji wa dawa umefikia asilimia 81 mwezi Juni 2023 kutoka asilimia 57 mwezi Juni 2022.
Bw. Tukai amesema kuwa pia wamefanikiwa kupokea shilingi bilioni 190.3 kwa mwaka wa fedha 2022/23 ikilinganishwa na sh bilioni 134.9 mwaka wa fedha 2021/22 ambapo sawa na asilimia 95.
“Ni hatua kubwa ambayo tumepiga katika utendaji kazi wetu , hakuna sehemu nilikwenda kuomba fedha nikakosa” amesema Bw. Tukai.
Amebainisha kuwa mapato kwa mwezi Agosti 2023 yameongezeka baada ya kupatikana shilingi bilioni 35.68 huku hali ya utendaji halisi shilingi bilioni 34.08.
Amesema kuwa wametekelezaji wa Mradi wa Ununuzi na Usambazaji wa vifaa vya huduma kwa wajawazito wanaopata uzazi pingamizi wakati wa kujifungua (CEmONC).
Amesema kuna Idadi ya vituo vya kutolea huduma vinavyopelekewa vifaa ambapo jumla ya vifaa vilivyopangwa kusambazwa 345, huku Idadi ya vifaa vilivyosambazwa hadi kufikia Juni 2023 ni 299 sawa na asilimia 87.
Bw. Tukai amesema kuwa gharama za Mradi wa thamani ya vifaa vinavyotarajia kusambazwa Tsh bil 99.7, thamani ya Vifaa vilivyosambazwa Tsh bil 79.4 sawa na asilimia 80 za utekelezaji.
Amesema kuwa pia wameanzisha kitengo maalumu cha usimamizi na ufuatiliaji wa mikataba ambapo ununuzi wa bidhaa za afya kutoka kwa wazalishaji wa ndani umeongezeka kutoka shil bil 14.1 mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia shil bil 39.77
“Hatujaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi zile ambazo zinakidhi mahitaji na viwango vya ubora hivyo kutegemea wazalishaji wa ndani, tumeanzisha zabuni maalumu zinazohusu wazalishaji wa ndani hivyo kuongezea uwezo wa uzalishaji” amesema Bw.Tukai.
Amesema kuwa pia kumeongeza idadi ya mikataba ya muda mrefu kutoka mikataba 100 yenye bidhaa za afya 711 kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia mikataba 233 yenye bidhaa 2,209 kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Ameeleza kuwa pia ujenzi wa wa Kiwanda cha mipira ya mikono “gloves” kilichopo Idofi, Njombe umekamilika pamoja na kuendelea kutambua sekta binafsi kwa maeneo ya uwekezaji ya bidhaa za afya za kimkakati za vidonge (tablets), rangi mbili (capsules), vimiminika nk, na bidhaa zitokanazo na zao la pamba na kutangaza matamanio ya ushirikiano kati ya MSD na sekta binafsi
“Kuna uanzishaji wa Kampuni Tanzu “MSD Medipharma Manufacturing Company Ltd” itakayosimamia uzalishaji wa bidhaa za afya” amesema Bw.Tukai.
Katika hatua nyengine amesema kuwa wameboresha ushirikiano na kuongeza ushawishi katika ngazi ya SADC Sekretarieti, na katika ngazi ya Nchi za SADC kupitia balozi zetu
“Tumeimarisha mifumo ya usimamizi kwenye ununuzi na usambazaji wa bidhaa za afya, ushirikiano na wadau wa mnyororo wa ugavi, kushirikisha balozi zetu zilizopo China, Algeria, Urusi na Korea ya Kusini kutafuta wadau wa uzalishaji na ununuzi” amesema
Pia wameboresha mifumo simamizi kwa kutumia TEHAMA mfano; mfumo wa usimamizi wa magari, kuanzisha kampuni tanzu ili kuweza kusimamia shughuli za uzalishaji wa bidhaa za afya kwa ufanisi, Ugatuzi wa Utendaji kutoka Makao Makuu kwenda Ofisi za Kanda.
Kuanzisha na kusimamia viwanda vya bidhaa za afya kwa kushirikiana na Sekta binafsi, Kuimarisha uhifadhi wa bidhaa za afya kwa kujenga maghala ya kisasa mikoa ya Kagera, Dar es Salaam na Mwanza.
Kusimika na kuimarisha matumizi ya TEHAMA kwenye kazi zote za Taasisi, Kuimarisha matumizi ya takwimu kwenye kazi zote, Kuimarisha mfumo wa usimamizi wa watendaji wa Taasisi, Kuongeza ushirikiano na wazalishaji wa ndani ili kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya.
Wameboresha Muundo wa Taasisi ili kuweza kuimarisha utendaji wa Taasisi, Ugatuzi wa shughuli zilizokuwa zinafanyika Makao Makuu kwenda Ofisi za Kanda, Kutumia vyanzo mbadala vya fedha ili kuongezea uwezo wa kifedha Taasisi.
Bohari ya Dawa (MSD) ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya, iliyoanzishwa mwaka 1993 kwa mujibu wa Sheria ya Bohari ya Dawa iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2021.