Na Sophia Kingimali.
Kutokana na kukua kwa teknolojia nchini wananchi wameaswa kutoa maoni chanya ili kuboresha sera ya TEHAMA ambayo itatumika katika kuleta maendeleo ya kidigital nchini
Hayo yamebainishwa leo Septemba 27 jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari, Selestine Kakele wakati akifungua kikao cha kutoa maoni kuhusu ya sera ya Taifa ya TEHAMA ambapo leo wamekutana na makundi anuai(makundi maalum) ikiwa ni muendelezo wa kukusanya maoni kwa makundi mbalimbali.
“Sera ya TEHAMA ya mwaka 2016 ni ya muda mrefu umepita na TEHAMA kama kiumbe ambacho kinazaliwa kinakua na kinabadilika kulingana na wakati na mambo mbalimbali yanatokea duniani katika jamii,”amesema Kakele.
Amesema wakati inatungwa sera hiyo mwaka 2016 hakukuwa na mambo ambayo leo yanatokea lakini yaliyokuwepo yalikuwepo hakukua na mtu angeweza kufasihi.
Amesema Teknolojia inakua kwa kasi sana ipo haja ya kufanya marejeo ya sera ya TEHAMA zipo taratibu za kuandaa sera moja ya shariti la msingi ni ushirikwishaji wa jamii.
“Tumekuwa na utaratibu huu tangu tunaanza mchakato wa kukutana na makundi mbalimbali na leo tumeona tukutane na makundi Anuai wenye changamoto mbalimbali za ulemavu lakini ni wadau wetu muhimu katika sera ambayo tunaifanyia mapitio,”amesema.
Aidha amesema sera hiyo itakapo kamilika itumike kujibu changamoto na kuwasaidia kutoa suluhisho la changamoto zinazowakabili watu kwenye makundi anuai(maalum) katika mlengo wa TEHAMA.
Ameongeza kuwa watawezeshaje taasisi za serikali na sekta binafsi zinazo husika na TEHAMA kuzingatia mahitaji maalumu katika utoaji huduma zao.
Aidha Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Nchini(SHIVYAWATA), Ernest Kimaya amesema sera ya TEHAMA ni muhimu kwa watu wenye ulemavu kutoa maoni ili kuboresha sera ambayo itazingatia makundi yote ya walemavu.
Naye Afisa Habari Chama cha Wachimbaji Wanawake Madini(TAWOMA) Halima Mhando amesema hakuna maendeleo yeyote bila mawasiliano kwa sasa hakuna kitu kinafanyika bila TEHAMA watatoa maoni yenye tija.
“Sasa hivi Dunia imebadilika kila kitu kinafanyika kidigital hivyo ni wakati sahihi wa sisi kama wadau ambao tunategemea kukuza shughuli zetu kupitia teknolojia kutoa maoni ili tuboreshe sera ya Tehama”