Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini, CP Awadhi Haji akiwasili katika ukumbi wa Polisi Jamii uliopo mkoani Dodoma alipopokelewa na Maofisa wa Jeshi la Polisi toka Makao Makuu kabla ya kuanza kikao kazi cha Maofisa wa Mkoa wa Dodoma na Wilaya zake zote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi (ACP) Martine Otieno akitoa taarifa fupi ya Mkoa kabla ya kumkaribisha Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Awadhi katika kikao kazi cha Maofisa wa Mkoa wa Dodoma pamoja na wilaya zake.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini, CP Awadhi Haji akizungumza na Maofisa wa Mkoa wa Dodoma na Wilaya zake zote (Wapo Pichani) katika kikao kazi chake ambapo aliwataka kuhakikisha wanakabiliana na kutokomeza uhalifu wa aina yoyote katika mkoa huo.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini, CP Awadhi Haji akiteta jambo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi (ACP) Martine Otieno baada ya kumalizika kikao kazi kilichowajumuisha Maofisa wa Mkoa wa Dodoma na wilaya zake.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini, Cp Awadhi Haji akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Mkoa wa Dodoma pamoja wilaya zake zote baada ya kumalizika kwa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Polisi Jamii mkoani humo.
(PICHA NA JESHI LA POLISI)