K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, KIBAHA
MKUU
wa Mkoa wa Pwani, Alhaj. Aboubakar Kunenge, amesema, utekelezaji wa majukumu ya
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), hususan katika kulipa fidia kwa
mfanyakazi aliyeumia au kufariki kutokana na ajali utatekegemea sana usahihi wa
taarifa za Jeshi la Polisi.
Mhe.
Alhaji Kunenge ameyasema hayo Septemba 26, 2023, wakati akifungua kikao kazi
baina ya WCF na Makamanda wa Polisi wa Usalama Barabarani wa Wilaya (DTOs)na
Wakaguzi wa Polisi wa Usalama Barabarani wa Wilaya za Mikoa ya Dar es Salaam na
Pwani, kilichofanyika mjini Kibaha.
“Kuna
wadau mbalimbali katika mnyororo wa WCF katika kuwahudumia wananchi na miongoni
mwa wadau hao ni Jeshi la Polisi, Kitengo cha Usalama Barabarani.” Alisema.
Alisema
kwa mujibu utaratibu wa utoaji taarifa kwa mfanyakazi aliyepata ajali ya
barabarani, Jeshi la polisi ndio lenye mamlaka ya kisheria kuthibitisha uwepo
wa ajali na kwamba taarifa hiyo ndiyo itatoa muongozo wa uchakataji wa madai
kabla ya muhusika kulipwa fidia.
Alisema
endapo Jeshi la Polisi halitafanya yale ambayo linapaswa kufanya katika
kuthibitisha ajali, mchakato mzima utakuwa umeharibika na kunakuwepo na
uwezekano wa kulipa fidia kwa mtu ambaye hastahili kulipwa na hivyo kupelekea
upotevu wa fedha za umma.
Akimkaribisha
mgeni rasmi kufungua kikao kazi hicho, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini WCF, Bw.
Emmanuel Humba, alisema, WCF iliingia makubaliano ya ushirikiano na Jeshi la
Polisi ili kurahisisha utoaji huduma kwa wnaanchi na hasa kuwezesha haki kutendeka
bila ya kuumiza upande wowote.
“Malipo
ya fidia hayawezi kufanyika bilaya taarifa sahihi kutoka Jeshi la Polisi
inapotokea ajali iliyomuhusisha mfanyakazi akiwa anatekeleza majukumu ya
mwajiri wake kwa mujibu wa mkataba wa ajira.” Alifafanua Bw. Humba.
Aidha
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini SACP. Ramadhani Ng’anzi
amewasisitizia Polisi wa Usalama Barabarani kuzingatia kanuni za kudumu za
Jeshi la Polisi, (Police General Order (PGO). Alisema, taarifa ya Jeshi la
Polisi lazima ieleze uhalisia wa tukio na si vinginevyo.
“Kwanafasi
yako ukiwa kama afisa wa polisi uadilifun ni jambo muhimu sana, nimesema uwe
ofisini au nje ya ofisi wananchi wameweka imani kubwa sana kwetu.” Alifafanua.
Kwa
upandew wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es
Salaam (ZTO), Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP. William Mkonda alisema, Makamanda
wa Kikosi cha Usama Barabarani wa Wilaya (DTOs) ni lazima wajenge tabia ya
kudodosa taarifa wanazopelekewa na askari wanaowaongoza.
“Tuwe
makini, tusome nyaraka zetu kabla hatujasaini, lakini huduma hizi tuzitoe kwa
wakati, PF90 inatumia wiki nzima mwananchi kuifuata kituo cha polisi? alihoji ACP Mkonda na kusisitiza
kuwa lazima huduma hiyo itolewe kwa haraka ili haki iweze kutendeka.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Mfanyakazi aliyeumia kutokana na
ajali anapaswa kutoa taarifa kwenye Mfuko, ndani ya miezi 12 tangu tukio hilo
litokee akiwa na taarifa ya polisi inayothibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Alhaj. Aboubakar Kunenge, akizungumza kwenye kikao akzi hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini WCF, Bw. Emmanuel Humba, akitoa nasaha zake mwanzoni mwa kikao hicho.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, SACP. Ramadhani Ng’anzi, akizunhuzma na makamanda hao
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Alhaji Aboubakar Kunenge (kushoto), akifurahia jambo na
Mwenyekiti wa Bodia ya Wadhamini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw.
Emmanuel Humba, (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu, WCF, Dkt. John Mduma,
(watatu kushoto), Mkuu wa Polisi wa Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Mwandamizi
wa Polisi, SACP. Ramadhani Ng’anzi (wakwanza kulia) na Kamanda wa Polisi Kikosi
cha Usalama Barabarani, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa
Polisi ACP. William Mkonda, baada ya ufunguzi wa kikao kazi baina ya Mfuko na
Makamanda wa polisi wa Usalama Barabarani wa Wilaya za mikoa ya Dar es Salaam
na Pwani na Wakaguzi wa Polisi kutoka mikoa hiyo. Kikao hicho kimefanyika
Kibaha, Septemba 26, 2023.
Baadhi ya makamanda wakifuatilia mafunzo hayo
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi
wa Polisi ACP. William Mkonda, akifafanua jambo wakati akitoa nasaha zake kwa makamanda hao
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Deus Sokoni, akitoa mada kuhusu umuhimu wa kuandika taarifa sahihi kwa ajili ya kuchakata madai ya fidia.