…..,………………..
Na. Sixmund Begashe
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba ameendelea kulinoa Jeshi la Uhifadhi (JU) kupitia warsha kwa Maafisa wa Jeshi hilo yenye lengo la kukumbushana masuala mbalimbali ya uhifadhi pamoja na masuala ya haki za kibinadamu.
Katika siku ya pili ya Warsha hiyo, Balozi Ltn Gen. Pau Mella, amewakumbusha Maafisa hao juu ya namna bora ya utatuzi wa migogoro na maridhiano kwenye utekelezaji wa majukumu, pamoja na umuhimu wa nidhamu mahala pa kazi, huku Bi. Elizabeth Wachuka, akifundisha juu ya umuhimu wa mawasiliano sahihi yanavyoweza kuchochoea ufanisi kazini.
Warsha hiyo itakayo dumu kwa siku tano, inawezeshwa na wawezeshaji nguli katika fani ya uongozi na yenye matarajio ya kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji ambayo yataleta Matokeo chanya kwa maslai mapana ya nchini.