Mkurugenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya Classic Pre &Primary iliyopo kata ya Sokon 1 ,Dk Reuben Makala akizungumza kuhusiana na mahafali ya while hiyo jijini Arusha
………………………………
Julieth Laizer ,Arusha.
Arusha .Serikali imeombwa kutoa ruzuku kwa shule binafsi kama ambavyo inafanya kwa shule za serikali ili kuziwezesha kuondokana na changamoto mbalimbali kwani wote kwa pamoja wanatoa huduma sawa kwa jamii.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mkurugenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya Classic pre and primary iliyopo kata ya Sokon 1 jijini Arusha,Dk Reuben Makala wakati akizungumza katika mahafali ya nne ya darasa la saba ambapo jumla ya wanafunzi 44 walihitimu masomo yao.
Amesema kuwa, shule binafsi zimekuwa zikikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo wanaomba serikali iwaunge mkono katika kutoa ruzuku kwa shule hizo kama ambavyo zinavyofanya kwa shule za serikali .
Aidha ameomba pia serikali kuwapatia walimu wa masomo mbalimbali ambao watakuwa wanalipwa na serikali kama ambavyo wizara ya afya inavyofanya ili kwa pamoja kuweza kushirikiana na kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
“Wengi wanadhani hii kazi tunayofanya tunapata faida kitendo ambacho wanapaswa kujua ni kutoa huduma tu kwa jamii lakini hakuna faida inayopatikana kama wengine wanavyodhani hivyo tunaomba sana serikali ituunge mkono ili tuweze kutatua changamoto mbalimbali.”amesema
Aidha Dk Makala alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kupunguza baadhi ya kodi kwani kumekuwepo na mlolongo mrefu wa kodi ambao wamekuwa wakitozwa shule binafsi hali ambayo inawaathiri pia katika utendaji kazi wao kwani kodi zimekuwa nyingi sana.
“Kuna mlolongo mrefu sana wa kodi tunazotozwa na serikali kiasi kwamba hata unajikuta hela yote unapata inaishia kulipa utitiri mrefu wa kodi jambo ambalo tunaomba serikali ilione hili na kulifanyia kazi kwa haraka.”amesema .
Aidha amesema kuwa ,shule hiyo ilianzishwa mwaka 2014 ambapo tangu kuanza kwa shule hiyo kumekuwepo na kiwango kikubwa sana cha ufaulu kwa wanafunzi shuleni hapo ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika masomo yao na kufaulu kwa kiwango cha A na B ambapo shule nzima ina wanafunzi 700.
Aa aye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ,Anold Ngowi amesema kuwa, shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika masomo yake kutokana na walimu waliobobea ambao wamekuwa wakifundisha kwa moyo na kwa vitendo zaidi kwa wanafunzi hao ili waweze kuelewa.
Ngowi amesema kuwa,tangu kuanzishwa kwa shule hiyo hadi sasa hivi kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hao kimekuwa juu sana huku wakiwafundisha wanafunzi hao kwa vitendo zaidi ili waweze kupata elimu ya tofauti na darasani.
Kwa upande wake mgenirasmi katika mahafali hayo,ambaye ni Mdau wa elimu Dk Albert Mbise ametoa wito kwa wazazi hao kuwekeza kwa watoto hao kwani ndio zawadi pekee wanayoweza kuwapatia na sio vinginevyo .
Amewataka wazazi hao kuwa mstari wa mbele kuendeleza ndoto za watoto wao badala ya kuwakatisha tamaa kwani wazazi wengi wamekuwa ndio kikwazo cha watoto kushindwa kufikia ndoto zao jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa katika jamii inayotuzunguka.
Kwa upande wa Mmoja wa wahitimu katika mahafali hayo ,Elizabeth Kumbi amewashukuru walimu hao kwa namna ambavyo wamekuwa wakiwasaidia wanafunzi hao kuweza kufaulu shuleni hapo na hata kuwajengea udhubutu wa kuweza kuwa wajasiri katika maswala mbalimbali .