Na Sophia Kingimali
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nauye amesema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kwenye sekta ya TEHEMA na Mawasiliano ili kusaidia kuleta maendeleo ya uchumi, kukuza biashara na kuongeza matumizi ya kidigitali katika kuimarisha sekta za kijamii kwani Dhamira ni kuongeza wigo wa mawasiliano na kuimarisha
Na Sophia Kingimali
Waziri wa habari mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nauye amesema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kwenye sekta ya TEHEMA na Mawasiliano ili kusaidia kuleta maendeleo ya uchumi, kukuza biashara na kuongeza matumizi ya kidigitali katika kuimarisha sekta za kijamii kwani Dhamira ni kuongeza wigo wa mawasiliano na kuimarisha huduma za intaneti ya kasi kuwafikia asilimia 85 ya Watanzania ifikapo mwaka 2025.
Hayo ameyasema leo Septemba 25 wakati wa utiaji saini wa Hati ya Maridhiano na Hati ya Mkataba wa nyongeza kati ya Wizara Ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Umoja wa Watoa za Huduma za Mawasiliano (Consortium of Telco Operators) ambao unajumuisha Kampuni ya Airtel Tanzania, Honora Tanzania (Tigo) na sasa Kampuni ya Vodacom Tanzania.
Amesema Dhamira ya Serikali kuingia Mkataba na Umoja huo ilikuwa ni kuongeza kasi ya kuyafikia maeneo yasiyokuwa na huduma za mawasiliano nchini kupitia jitihada za pamoja na Sekta binafsi za ujenzi wa mkongo ambapo Utekelezaji wa Mkataba huo ulikumbwa na changamoto mbalimbali ambazo zilipelekea pande zote mbili kukutana, kujadiliana na hatimaye kufikia muafaka.
“Leo hii tumeshuhudia utiaji saini wa Hati ya Maridhiano (Deed of Settlement) ambapo Consortium imeridhia kutoa fedha taslim dola za Marekani milioni 20 ambazo ni takribani Shilingi Bilioni 50 kwa kipindi cha miaka 5 ikiwa ni malipo ya matumizi ya njia za miundombinu hiyo toka ilipojengwa hadi sasa pamoja na kufanya uwekezaji wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 13 sawa na takribani shilingi Bilioni 32.5.
Pia tumeshuhudia utiaji saini wa Hati ya Mkataba wa Nyongeza (Addendum of Memorandum of Agreement) ambapo Kampuni ya Vodacom Tanzania imekuwa sehemu ya Conosrtium , hali inayoonyesha ushirikiano uliopo kati ya Sekta binafsi katika kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi nchini”amesema.
Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaendelea kusimamia sekta ya mawasiliano na TEHAMA nchini na kuhakikisha mawasiliano yanawafikia watanzania wote, ikiwa ni mkakati wa Serikali kuhakikisha wananchi wote wanapata mawasiliano ili kuleta maendeleo nchini.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa TEHAMA, Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa watoa huduma na wawekezaji kujenga Miundombinu ya Mawasiliano nchini kote.
“Hivi karibuni mlishuhudia utiaji saini mradi wa kujenga minara mipya 758 ili kuongeza na kupanua wigo wa mawasiliano (coverage) ambayo itawafaidisha zaidi ya watanzania milioni nane kote nchini. Pia Serikali imepunguza gharama za kuweka miundombinu ya mkongo kutoka Dola za Marekani 1000 hadi 100 ili kuharikisha ufikishaji wa mawasiliano bora kwa wananchi. Vilevile Serikali imeongeza uwezo wa Mkongo wa Taifa kutoka kwenye uwezo wa 200Gbps hadi kufikia 800Gbps na inaendelea na upanuzi huo kufikia kiwango cha 2000Gbps sawa na 2Tbpsc”amesema Nape.
Pia amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa Mkongo wa Taifa ambao unatarajia kufikia Wilaya 99 kati ya 139 ifikapo mwezi Machi Mwakani huku lengo likiwa ni kufikia wilaya zote 139 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2024.
Amesema Serikali itaendelea kuwekeza kwenye ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kufikia Wilaya zote na kuhakikisha una uwezo wa kutosha wa kutoa mawasiliano kwa ubora, gharama nafuu na uhakika Pia kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa Watoa Huduma wote kuendelea kujenga na kutoa huduma za mawasiliano nchini.
Amesema lengo la serikali kuona nchi inapiga hatua katika kuongeza kasi ya matumizi ya mifumo ya kidijitali kwa kuwa kuna miundombinu ya kisasa ya TEHAMA na Mawasiliano inayopitisha mawasiliano kwa kasi na ubora stahiki.
Aidha Nape ameitaka Wizara yake kusimamia vema utekelezaji wa Mikataba hiyo pamoja na kuharakisha ukamilishaji wa mkataba wa uwekezaji.
“Naelekeza Wizara, Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Consortium kukamilisha mkataba wa Haki ya Matumizi wa Miundombinu hiyo ambao utawezesha miundombinu kutumika kwa ubora na usawa uliokusudiwa”amesema.
Aidha Nape ametoa rai kwa Watoa Huduma za Mawasiliano kuendelea kuwekeza kwenye miundombinu inayowezesha kufikisha huduma kwa watumiaji wa mwisho ambao ni wananchi kwani eneo la uwekezaji bado kubwa na linahitaji uwekezaji wa pamoja kufikia malengo ya Taifa.
“Mwelekeo wa Serikali ni kuona kuwa Tanzania ya Kidigital inafikiwa na matokeo yake chanya yanasaidia kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi na shughuli za kijamii kwa kutumia TEHAMA”amesema Nape.
Tarehe 04 Oktoba, 2011 Serikali kupitia iliyokuwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia iliingia Makubaliano ya miaka thelathini (30) na Umoja wa Watoa Huduma za Mawasiliano uliokuwa unajumuisha kampuni ya Celtel Tanzania LTD (Airtel), MIC Tanzania LTD (Tigo) na Zanzibar Telecom LTD (Zantel). Mkataba huo ulihusu ujenzi wa mkongo wa mawasiliano (Optic Fibre Cable Network) wenye njia arobaini na nane (48-Cores) katika maeneo yaliyokuwa hayajafikiwa na Mkongo wa Taifa (missing links).
huduma za intaneti ya kasi kuwafikia asilimia 85 ya Watanzania ifikapo mwaka 2025.