Benki ya NMB imezindua rasmi hati fungani ya jamii bond ya muda wa Kati na muda. Mrefu yenye jumla ya shilingi trilioni moja.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa hati fungani hiyo mpya nchini katika uzinduzi uliofanyika jijini Da es Salaam Leo Septemba 25,2023. Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna amesema Jamii Bond inadhamira ya kukusanya fedha zitakazowawezesha kutoa mikopo inayolenga kuleta matokeo chanya kwenye jamii kupiyltia miradi mbalimbali ikiwemo ya mazingira,wanawake na vijana pia miradi inayolenga kuhakikisha usalama wa chakula ,nyumba za bei nafuu, afya, na elimu.
Aidha Bi Ruth Zaipuna amesema Jamii Bond inatoa muda wa uwekezaji wa miaka mitatu na itatoa riba ya 9.5%kwa mwaka na italipwa mara nne kwa mwaka huku kiwango cha uwekezaji kikianzia shilingi laki Tano .
Hata hivyo Bi Ruth amesema lengo kuu la Jamii Bond ni kukusanya shilingi bilioni 75 huku mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA)ikiruhusu ongezeko la mpaka shilingi bilioni 25 na kutoa idhinisho la dola za kimarekani milioni 10 na kuruhusu ongezeko la Dolla million Tano na kufanya kuwa na jumla ya Dolla million 15 iyakayouzwa kwa mashirika na wawekezaji walioko nje ya Tanzania.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na wataalam mbalimbali wa masuala ya kifedha akiwemo msajili wa hazina,Afisa mtendaji mkuu wa soko la hisa,Mtendaji mkuu wa mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA)huku hati fungani hiyo ya Jamii Bond inatarajiwa kuleta Chachu katika soko la hisa pamoja na ushindani wa hati fungani Afrika mashariki.