Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Emmanuel Tutuba akipata maelezo kutoka kwa Bi. Lucy Kelvin Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati alipotembelea banda la Benki hiyo katika maonesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Emmanuel Tutuba akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Mifumo na Malipo Bw. Ephraim Madembwe wakati alipotembelea katika banda la benki hiyo kwenye maonesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Emmanuel Tutuba akitoa maelekezo kwa Meneja Msaidizi, Upatikanaji na Usimamizi wa akiba ya Fedha za kigeni nchini, Dkt. Anna Lyimo wakati alipotembelea katika banda la benki hiyo kwenye maonesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Geita, Cornel Maghembe kulia wakati walipokutana katika maonesho ya madini Geita,kushoto ni Meneja wa Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania BoT Victoria Msina.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Emmanuel Tutuba akipata maelezo kutoka kwa Revocatus William mchambuzi wa mifumo BoT wakati alipotembelea katika banda la benki hiyo kwenye maonesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Emmanuel Tutuba akipata maelezo kutoka kwa Kadee Mshihiri Afisa Mwandamizi mkuu katika Kurugenzi ya Mifumo ya malipo Benki Kuu ya Tanzania BoT wakati alipotembelea banda la BoT katika maonesho ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Emmanuel Tutuba akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigella wakati alipotembelea katika maonesho ya madini mjini Geita.
Na Mwandishi wetu
Gavana wa benki kuu(BoT)Emmanuel Tutuba amesema kilo 418 za dhahabu zilizonunuliwa na serikali kutoka kwa wachimbaji na kusafishwa na viwanda vya ndani tayari zimepelekwa London nchini Uingereza ili kusajiliwa kwenye soko la kimataifa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza kutembelea Banda la Benki hiyo kujionea shughuli wanazofanya katika maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Bomba mbili – EPZA Mkoani Geita Leo, Septemba 23 ,2023.
“Tayari kwa mara ya kwanza tangu Tanzania ipate uhuru tulikuwa tunatunza na kuhifadhi fedha za kigeni ikiwemo Dola lakini kwa mara ya kwanza sasa imengia kwenye historia ya nchi zinazo hifadhi dola zetu kwenye dhahabu ambayo imenunuliwa Tanzania,”amesema.
Amesema wadau mbalimbali Wafike kwenye maonesho ili kupata elimu na wataendelea kuhamasisha wananchi watumie zaidi mifumo ya kielektoniki kufanya malipo kwa sababu ni ya haraka na salama.
Amesema bado wadau wanahitaji kufahamu masuala mbalimbali ikiwemo namna BOT inashiriki kwenye sekta ya madini.
“Kwanza sisi kama BoT kwa dhamana tulionayo ya kusimamia masuala ya ukuaji wa uchumi na uhimilivu wa bei pamoja na mzunguko wa fedha na thamani ya fedha tupo hapo kwa ajili ya kuhabarisha wananchi lakini pia kushirikiana na taasisi mbalimbali na wachimbaji au wadau wa masuala ya madini,” amesema Gavana Tutuba.
Amesema wao wamefika katika maonesho hayo ikiwa ni mojawapo ya mikakati yao ya kutoa elimu na kushiriki katikati ukuaji wa uchumi.
Ameeleza kuwa a idara mbalimbali zimeshiriki ikiwepo Chuo Kikuu cha Benki ambacho kipo Mwanza lakini kuna baadhi ya idara zinazosimamia sekta ya fedha uchapishaji wa fedha na wengine wanasimamia mifumo ya malipo, uwekezaji wa mitaji kwenye dhamana za serikali na hati fungani.
Pia wengine wanasimamia masuala ya tafiti na bei za bidhaa mbalimbali ikiwemo bei za madini kwa hiyo wako hapo wakiangalia shughuli zote wao kama BoT ni wadau wakubwa hivi sasa wameanza kununua dhahabu kama walivyosikia kwenye hotuba ya Waziri wa Fedha serikali itaanza kununua dhahabu.
Amesema bado wanaendelea kununua na wamejipanga kununua kwa wachimbaji wadogo, kati na wakubwa na kwa wale wauzaji ambao wapo maeneo mbalimbali.
Amesema hivi sasa walipofika kwenye maonesho hayo wanaendelea kuhamasisha watu waje kupata elimu na wafahamu namna ambavyo wanaweza wakauza dhahabu yao kupitia BOT.
Amesema na wao kwasababu wananunua wanatoa bei halisi ya soko kwa siku hiyo tofauti wengine ambao wamesikia wananunua kwa bei za chini zinawekana haziwapi manufaa makubwa wananchi.
Tutuba amesema kuwepo kwao wanaendelea kuwafahamisha na kuwaelimisha wananchi kuhusu Mifumo yao ya kudhibiti uhalifu kwa sababu wanafahamu wachimbaji na wadau mbalimbali wa madini wanapokea fedha nyingi au wanatumia fedha tasilimu katika miamala ya kulipa au kupokea.
Amesema wao kama BoT wametengeneza Mifumo ya kurahisisha wana mfumo unaitwa Tanzania Payment System maarufu kama Tips.
Amesema mfumo unarahisisha kwa sababu umeunganishwa mabenki yote na watoa huduma wa miamala kwa njia ya kampuni za simu.
Kwa kutumia mfumo huo umepunguza gharama za kuhamiasha miamala kutoka Kampuni moja kwenda nyingine au kubadilishana kutoka benki moja kwenda nyingine.
Amesema bado wanahamasisha wadau wa uchimbaji madini watumie zaidi miamala ya kieletroniki kuliko kutumia fedha tasilimu.
Amesema hiyo itasaidia kuepukana na kupata fedha bandia wamesikia kuna baadhi ya maeneo zipo na timu za ufuatiliaji zinaendelea kufuatilia watakapo baina wanachukua hatua.
Aidha amesema wachimbaji wa madini waje kuwekeza hati fungani na dhamana za serikali katika uwekezaji huo utaendelea kupata faida ya asilimia iliyotengwa ya riba ya karatasi utakayopewa.
“Ni mkataba ambao ni uhakika kwa sababu hazina hatari yeyote kupata riba kila baada ya miezi sita,”amesema.
Amewashauri wawekezaji wa madini wapate elimu namna ya kufanya uwekezaji huo kwa tija na kupata manufaa zaidi.