Na Sophia Kingimali
Mbunge wa Morogoro Mjini Abdul Abood amewataka wasimamizi wa fedha za miradi ya uboreshaji wa Miundombinu ya Halmashauri za Miji na Manispaa Mkoani Morogoro ambayo imetolewa na serikali kuhakikisha fedha hizo zinafanya kazi iliyokusudiwa na si kuishia kwa watu kwani ameahidi kusimamia kwa ukaribu kwani hatakua tayari kuona fedha hizo zinaliwa na wajanja.
Mbunge huyo ametoa kauli hiyo septemba 23 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kumalizika Kwa hafla ya kutiliana saini Mikataba 12 ya awali ya Miradi ya Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji ya Tanzania(TACTIC) ambapo Mkoa wa Morogoro umetengewa fedha Dola laki 751,000 sawa na bilioni Tsh.Bilioni 19,606,559,115.00 kwa ajili ya uboreshaji wa Miundombinu hiyo.
Fedha hizo zitatumika katika kuboresha na kujenga Barabara za lami,,Masoko ya kisasa,Madaraja ,kuweka taa za barabarani ikiwa lengo ni kuweka miji na Manispaa za Mkoa huo kuweza kukuza uchumi wa Taifa pamoja na mtu mmoja mmoja kutokana na kufanya shughuli za uchumi bila usumbufu.
“Namshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada alizozifanya za kutafuta fedha kwa ajili ya kuboresha Miundombinu katika Majiji na halmashauri zetu,Mimi kama Mbunge wa Morogoro Mjini nitahakikisha nafuatilia fedha hizi kwa ukaribu kuona kama zimeweza kutumika vizuri katika kutekeleza miradi iliyokusudiwa ‘amesema Mbunge Abood.
Serikali imepata Dola Milioni 410 bila VAT ikiwa ni Mkopo wa Benki ya Dunia (lDA19) kwa ajili ya mradi wa kuboresha miundombinu ya miji ya Tanzania(TACTIC) ambapo mradi huo itatekelezwa kwa awamu tatu,ambazo awamu ya kwanza ni Miji 12 katika mwaka huu wa Fedha 2020/2024,kundi la pili ni Miji 15 huku kundi la tatu ni Miji 18 litaanza utekelezaji mwaka wa Fedha 2024 /25 ambapo muda wa utekelezaji utakua miaka sita kuanzia mwaka wa Fedha 2022 / 2023 ambapo jumla ya miji 45 inatarajiwa kunufaika na mradi huo.