Mkuu wakoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila akizungumza katika kikao kazi kati ya Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF ma Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi. mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Bw. Adam Fimbo akizungumza katika kikao kati ya Wahariri wa vuombo vya habari TMDA Leo jijini Dar es salaam.
Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Bi. Gaudensia Simwanza akifafanua mambo kadhaa katika kikao. Kazi hicho..
Na Sophia Kingimali
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kutumia taaluma wakati wa uhariri wa habari zao na si mihemko ili kuhakikisha habari zinazotolewa kuwa zenye tija, haki na usawa.
Hayo ameyasema leo wakati akifungua kikao kazi kilichoandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) kwa wahariri wa wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Amesema kutokana na kukua kwa teknolojia katika sekta ya habari umakini zaidi unahitajika katika kuhabarisha umma ili kuepuka uvumi au uchochozi hali ambayo inaweza kuchafua utu wa mtu au Taifa.
“Hapa ni seme tu ukweli tunapaswa kutumia teknolojia katika kuhabarisha tunapaswa tujue mwananchi anapenda kusikia nini tutumie njia hizo hizo lakini kwa kutumia taaluma ili kuhakikisha ujumbe ulioukusudia unafika”amesema Chalamila.
Aidha ameongeza kuwa vyombo vya habari vya mtandao vinapaswa kutumia taaluma pia katika uhariri kwani taarifa nyingi zinazotolewa kutumia vyombo hivyo zinakuwa hazina uwiano.
“Teknolojia imekua sasa unakuta mwenye blog ndio muandishi na ndio muhariri si dhani kama ni Sawa na wao wanapaswa kutumia taaluma katika kuhabarisha ili waendelee kuaminika”ameongeza Chalamila
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo amesema kuwa mafanikio makubwa yaliofikiwa na mamlaka hiyo imetokana na juhudi zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kutendea kazi.
Amesema serikali imewezesha TMDA kuwa na vifaa ambavyo vinaweza kufanya kazi kwa haraka na kutoa Majibu ya uhakika hali ambayo inasaidia kulinda afya za wananchi.
Amesema sasa hivi Tanzania imeanza kutoa huduma ya upimaji wa dawa kwa nchi mbalimbali kwani wamekua wakileta sampuli za dawa nchini ili kuweza kupimiwa.
Serikali imefanya uwekezaji mkubwa Sana ili kuhakikisha afya za watanzania zinaboreka lakini pia uingizwaji wa dawa zisizo na ubora nchini unaisha”amesema Fimbo.