Na Ashrack Miraji
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro kwa kauli moja wamepitisha rasimu ya sheria Ndogo ya mahudhurio ya lazima na Upatikanaji wa chakula shuleni kudhibiti utoro kwa wanafunzi kwenye shule zote za msingi na Sekondari wilayani humo pia waweze kuwa na afya Bora.
Akiwasilisha rasimu hiyo kwenye kikao cha baraza la madiwani, Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Upendo Kivuyo amesema sheria hiyo imelenga kuboresha afya za wanafunzi ili kuimarisha uelewa wao wawapo shuleni.
Kwa upande wake katibu tawala msaidizi wa utawala wa Fedha, usimamizi na ukaguzi ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro Prosencian Kirumbi amepongeza usimamizi mzuri wa Halmashauri hiyo kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato uliofanya kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo.
“Nitoe pongezi kwa viongozi wa Wilaya ya Same kwa kuonesha upendo na mshikamano kwenye utekelezaji wa majukumu yenu nikiamini ndio uliowawezesha kupata mafanikio yanayoonekana hasa kwenye usimamizi wa Miradi na Upande wa kukusanya mapato”. Amesema Kirumbi.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Same Kaslida Mgeni amewata madiwani wa Halmashauri hiyo ya Same kuwa mabalozi kuendeleza kampeni yake ya kupambana na Dawa za kulevya hasa Kutokomeza Kilimo cha Mirungi na biashara haramu ya zao hilo kupinga kwa kutumia nafasi zao kutoa elimu ya madhara yake kwa wananchi kila wanapokuwa kwenye mikutano yao kwenye jamii.
“Pamoja na ushirikiano mzuri tulionao kwenye kusimamia na kutekeleza Miiradi na kukusanya Mapato niendelee kuwaomba waheshimiwa Madiwani mniunge mkono kwenye mapambano ya kutokomeza Dawa za kulevya kwani jambo hili ni baya na madhara yake wote tunayajua”.Alisema Kasilda Mgeni Mkuu wa Wilaya ya Same.
Amewasihi pia wakazi wa wilaya hiyo kudumisha upendo, amani na mshikamano kama anavyo sisitiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani akisema ndio njia pekee kujenga Uchumi wa nchi na kueleta maendeleo.
“Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani ametupatia Fedha nyingi za Miradi kwenye wilaya yetu ya Same ikiwemo kufanikisha mradi mkubwa wa kuboresha huduma ujenzi wa Hospital kubwa ya kisasa inayogharimu zaidi ya shilingi Bilioni saba lazima tumuunge mkono kama sehemu ya kurejesha fadhira kwenye serikali yake”. Alisema mkuu huyo wa Wilaya.
Mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya Same Anastazia Tutuba ameahidi kuendelea kusimamia miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye eilaya hiyo ikiwemo miradi ya kuboresha huduma inayoibuliwa na wa wananchi pamoja na miradi mingine ya kimkakati iliyopewa fedha na serikali.
MWISHO. rasimu ya sheria Ndogo ya mahudhurio ya lazima na Upatikanaji wa chakula shuleni kudhibiti utoro kwa wanafunzi kwenye shule zote za msingi na Sekondari wilayani humo pia waweze kuwa na afya Bora.