Na Ahmed Mahmoud
Waziri wa Elimu Sayansi na mafunzo ya Amali Prof. Adolfu Mkenda ameeleza kuwa Wakaguzi wa ndani ni kada muhimu inayosaidia maafisa masuhuli kudhibiti matumizi ya fedha za serikali.
Prof.Mkenda ameyasema wakati akifungua Mkutano wa16 wa bodi ya Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani IIA unaofanyika kwa siku tatu Jijini Arusha na kuwataka Wakaguzi hao kufanyakazi zao kwa weledi sanjari na maslahi ya mapana taifa lao.
Alisema kwamba wakati akiwa Afisa masuhuli aliona umuhimu Mkubwa sana wakuwatumia Wakaguzi wa ndani kuweza kujua sehemu gani inaleta shaka ili kuweza kuweka sawa kwa sababu suala Kubwa hapa sio kusubiri ubadhirifu au upotevu wa Mali ya umma utokee ndio tuchukuwe hatua mara nyingi tudhibiti haraka.
Aidha alisema kuwa Wakaguzi wa ndani wakitumika ipasavyo inasaidia kuchukuwa hatua za haraka kabla ya upotevu wa fedha za miradi na kuwataka kuwa chachu ya maendeleo na Usimamizi wa miradi ya serikali bila kungoja kuitwa.
Awali akimkaribisha Waziri Prof. Mkenda Naibu Waziri wa Fedha Hamad Chande amewataka Wakaguzi wa ndani kutokubali kuachwa nyuma na badala yake kuchukuwa hatua za Ufuatiliaji wa matumizi sahihi ya fedha za umma kwa kuelekeza kabla hayajatokea madhara.
Amesema kwamba zoezi Zima la mchakato wa Taasisi za umma na binafsi lazima wawashirikishe Wakaguzi wa ndani ili kuleta matokeo ya haraka na kuokoa fedha za umma iwapo watashirikishwa kuanzia mwanzo.
Kwa Upande wake Rais wa Umoja wa Taasisi ya Wakaguzi wa ndani IIA CPA Zelia Njeza amesema Hadi Sasa Tanzania haijafanya vizuri katika suala Zima la uanachama na kutoa wito kwa Wakaguzi wote wanaofanya Kazi za Ukaguzi wa Ndani waweze kujinga na Taasisi hiyo ya IIA.
Alibainisha kwamba Moja ya Maslahi mapana ya kuwa mwanachama ni pamoja kusaidiwa pale unapokuwa na changamoto ya kikazi sanjari na kupata hati ya kitaifa na kimataifa ya kutambuliwa pia inakuunda vizuri katika utendaji wako wa Kazi lakini kwa wale Wakaguzi wasio wahasibu wanaweza kupata misingi ya Taaluma nzima.
Hata hivyo Mkaguzi Mkuu wa ndani wa SMZ Fatma Khamis Mohammed amesema kwamba kada hiyo ikitumika vyema kwa weledi na nidhamu chini ya IIA itasaidia sana kuboresha Usimamizi wa miradi ya maendeleo sanjari na mashirika yetu.