Na Sophia Kingimali
Ili kuendelea kukuza vipaji vya vijana katika sekta ya mpira wa miguu kampuni ya bia ya safari imezindua kampeni ya kusaka vipaji nchi nzima lengo likiwa kuzalisha vipaji vipya nchini huku mshindi wa michuano hiyo kuibuka na kitita cha milion 44.
Akizungumza Leo septemba 19 jijini Dar es salaam wakati akizindundua kampeni hiyo meneja chapa ya Safari Lager Pamela Kikuli amesema mashindano hayo yatafanyika mikoa mbalimbali ambapo baada ya mashindano itaundwa timu itakayojulikana kama safari champions yaani mapigwa wapya katika mpira.
“Tumeamua Kuja na kampeni na kampeni hii ili kuibua vipaji vipya kabisa vya mpira wa miguu kwani tunaamini Kuna vipaji vingi nchini ambavyo avijaibuliwa”amesema Kikuli.
Amesema mashindano hayo yatafanyika katika mikoa minne ambayo ni Mbeya,Arusha,Mwanza na Dar es salaam huku mkoa wa Kwanza ukiwa mbeya ambapo mashindano hayo yatafanyika katika viwanja vya FFU Polisi octoba 7.
“Timu zile za mikoa zitatumika kuchagua vijana ambao wataunda timu moja kubwa ya wachezaji 22 ambao watacheza mechi ya kirafiki na timu mojawapo ya ligi kuu.”amesema
Ameongeza kuwa mchezaji mmoja kati ya Hao atapata fursa ya kuchaguliwa na mawakala wa ligi kuu Bara ili kuweza kuchezea timu kubwa baadae.
Amesema timu hiyo ya safari champions itakayocheza na timu ya ligi kuu itajinyakulia kitita cha million 44 kama kifuta jasho kwa ajili ya michuano hiyo.
“Hii michuano si midogo itakua na change changamoto nyingi hivyo tutawazawadia hao washindi kiasi hiko cha pesa ili kuendelea kuwapa motisha”ameongeza.
Kwa upande wake kocha Jamuhuri Kihwelo ambae ndio ataendesha mchakato kwa kushirikiana na Sekilojo Chambua amesema mchakato huo utakua wa wazi na wala hautakua na upendeleo wowote hivyo vijana wajitokeze kwa wingi ili kushiriki mchuano hiyo.
Nae kocha Sekilojo Chambua amesema uwepo wa michuano hiyo ni mapinduzi katika sekta ya mpira Kwani itasaidia kuibua vipaji vipya ambavyo vitakua rasilimali kwa nchi.
“Tukiwa na wachezaji wetu wenye viwango hapa nchini wataweza kwenda kucheza hata soka la kulipwa nje na hii itakua ni heshima kwa taifa”amesema Chambua”