Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan leo mchana anatarajia kuweka jiwe la Msingi Hospitali ya Rufaa Lindi (MITWERO), ambayo kwa hadhi yake inafanana kabisa na Hospitali zingine kubwa Kama Muhimbili ya Dar es salaam.
Aidha wananchi wa Mkoani humo wamefurahishwa sana na jitihada hizo za Mhe.Rais kuwajengea Hospitali hiyo kubwa na kupunguza kero waliyokuwa wanaipata hapo Mwanzo kusafiri nje ya mkoa kupata huduma ya matibabu kwa yale Magonjwa Sugu.