Jeshi la Polisi mkoani Manyara limefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya Mirungi bunda 250 na bangi misokoto 897 katika wilaya za Simanjiro na Kiteto.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara George Katabazi Mtuhumiwa anayeshikiliwa ni Richard Dhahabu (61) mkazi wa kijiji cha Ngage wilayani Simanjiro aliyekamatwa usiku wa tarehe 16,2023 akiwa na bangi hiyo.
Aidha Katabazi amesema tarehe 17,2023 asubuhi katika Kijiji cha Namelok wilaya Kiteto, bara bara ya Kongwa-Dodoma walikamata dawa za kulevya aina ya Mirungi bunda 250 ikisafirishwa kwa pikipiki isiyokuwa na namba za usajili ili wasifahamike.
Amesema taarifa za siri walizopata zilisaidia kufuatilia watuhumiwa hao ambapo walipogundua wanafuatiliwa walikimbia kwa kasi hali iliyosababisha kupata ajali baada ya kugonga jiwe na kupelekea kifo cha dereva aliyekuwa akiendesha Mkacha Mohamedi (35) ambaye alifariki akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kiteto huku mwenzake Nassibu Yahaya 23 akiendelea kushikiliwa kwa mahojiano zaidi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Geoge Katabazi ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kuachana na biashara ya dawa za kulevya na badala yake wafanye kazi zingine halali kwani dawa hizo zinamaliza nguvu kazi ya taifa ambao ni vijana.