………………
Adeladius Makwega-MWANZA
Wakristo wametakiwa kuwa watu wa msamaha na huko kunatokana na mapungufu ya kila mmoja wetu na kutokana na huo msamaha ndipo Baba Yetu wa Mbinguni atatusamehe na sisi kila mmoja makosa yake.
“Huika ya binadamu ni kupokea mazuri kutoka kwa wengine lakini ana tabia ya kupuuza mambo ya wengine, jambo hilo linakosesha fursa ya kutambua kuwa na sisi siyo wakamilifu wa kutosha, tunaendelea kuishi katika mazingira yetu kwa kuwa wapo wanaotusamehe.
Jiulize je dominika hii na wewe upo tayari kuwasamehe wengine? Je upo tayari kutoa nafasi nyingine kwao ? Hayo ndiyo mafundisho ya masomo yote ya dominika ya leo.
”Hayo yamesemwa na Padri Samson Masanja katika Misa ya dominika ya 24 ya Mwaka A Liturjia ya Kanisa , jumapili ya Septemba 17, 2023, katika Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Wamisionari, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza katika Misa ya Kwanza ya dominika hii iliyoanza saa 12 kamili ya asubuhi.
Akiendelea kuhubiri katika misa hiyo Padri Masanja alisema kuwa mtu ambaye ana hasira anaweza kufanya ubaya wowote ule zaidi lakini akikubali kusamehe anakuwa na amani.
Kila mmoja ajiulize moyo wake umejaa nini? Je ni hasira, moyo wa kisasi, ghadhabu, Je ni chuki au ubinafsi ?“Hayo yanamkosesha Mkristo kuwaona wengine wanahitaji msamaha. Jiulize huu ni mwaka wa ngapi haujasamehe aliyekukosea, je wa kwanza, wa pili, wa tatu au mwaka wa kumi?
”Padri Masanja ambae pia ni Paroko wa Parokia ya Malya, akiendelea kuhubiri katika misa hiyo, huku akichanganya Kiswahili na Kisukuma , Malya likiwa eneo lenye Wasukuma wengi alisema kuwa wapo ndugu zetu hawasamehi hadi wanapatwa na magonjwa mbalimbalim, kisa cha hayo ni kubeba hasira, kisa ni chuki, hawana msamaha kabisa .
Yesu anasema msamaha hauna kikomo ambapo ni saba mara sabini na wala haupaswi kuhesabu uliokosewa.Padri Masanja akiongoza misa hiyo iliyokuwa na mafrateli wawili na makatekista wawili alirejea nyimbo mbili akianza na wimbo wa katikati wa dominika 24 ya mwaka A,“Bwana amejaa huruma na neema, si mwepesi wa hasira . Ni mwingi wa fadhili.
”Pia alirejea maneno ya wimbo wa Kwaresma ,“Bwana kama wewe ungehesabu maovi yetu, nani angesimama, nani angesimam,a nani angesimama mbele yako?”Misa pia iliambata na nia na maombi kadhaa,“Tunawaombea wale wanaoshika nafasi katika mahakama na magereza wawe na moyo wa utu kwa wafungwa magerezani, Ee Bwana- Twakuomba Utusikie.
”Hadi misa hiyo ya kwanza inamalizika, hali ya hewa ya eneo la Malya na viunga vyake, kwa juma zima ni jua la kadili , mvua haikunyesha kabisa, ambapo mwandishi wa ripoti hii bado anajiuliza je zile mbegu za wakulima wachache waliopanda mashambani wakiamini masika imewadia je zitakuwa bado ziko salama ardhini?