Vijana wa Bodaboda mkoa wa Lindi siku ya leo wameamka na shangwe la kutosha yote ikiwa ni furaha ya ujio wa Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anayetarajia kuingia Mkoani humo kwa ziara ya siku tatu.
Aidha vijana hao wametoa shukrani zao kwa Mhe.Rais kuweza kuwapunguzia Faini ya pikipiki kutoka elfu 30,000 hadi elfu 10,000 nchi nzima pia kumekuwa na urafiki kati yao na Trafiki barabarani.