Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Biteko akiwasili katika uwanja wa ndege kwa ajili ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) leo Septembe 16, 2023 Rufiji mkoani Pwani, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Bw. Maharage Chande.
……………………………………
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Biteko amewapongeza wakandarasi wanaojenga mradi wa bwawa la kuzalishia umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP) kwa kufanya kazi kwa kasi ili kuhakikisha tatizo la umeme linakwisha nchini.
Akizungumza wakati mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia 91.72 amesema kukamilika kwa mradi kwake kutasaidia kumaliza tatizo la umeme nchini.
“Nipende tu kuwaambia watanzania tatizo la umeme tulilonalo ni la muda mfupi na litaisha hivyo tutakua na umeme wa uhakika kwa sababu bwawa linaendelea kujaa kwa kiwango kilichotakiwa”amesena Dkt Biteko
Amesema mradi huo umegaharimu kiasi cha shilingi tilion 6.6 ambapo mkandarasi wake tayari ameshalipwa asilimia 88.5 ya malipo yake.
Amesema mpaka kufikia hapo ni juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa mradi huo katika kuhakikisha shughuli za uchumi hazikwami kutokana na ukosefu wa umeme.
“Nipende kumshukuru Sana Rais wetu Dkt Samia kwa maana ameweka juhudi kubwa ili kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi”amesema
Amesema ukosefu wa umeme umetokana na uhaba wa maji katika vyanzo vya kuzalishia umeme
“Tupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha mradi ili tuweze kupata umeme wa maana zaidi na kuwasaidia watanzania kukuza uchumi wao katika shughuli zao za uzalishaji”amesema Biteko.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Biteko akisalimiana na watendaji mbalimbali na wahandisi wakati alipowasili katika uwanja wa ndege kwa ajili ya kukagua ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) leo Septemba 16, 2023 Rufiji mkoani Pwani, kutikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Bw. Maharage Chande.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Biteko akisikiliza maelezo kutoka kwa Emanuel Mwandambo Mhandisi Mshauri Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) ambapo ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 91% wakati alipotembelea mradi huo leo Septembe 16, 2023 Rufiji mkoani Pwani, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Bw. Maharage Chande.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Biteko akisikiliza maelezo kutoka kwa Emanuel Mwandambo Mhandisi Mshauri Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) ambapo ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 91% wakati alipotembelea mradi huo leo Septemba 16, 2023 Rufiji mkoani Pwani, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Bw. Maharage Chande.
Msafara wa Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Biteko ukiwasili katika eneo la ujenzi wa Tuta kubwa la kuzuia maji (Darm) ili kujionea shughuli ya ujenzi inavyoendelea.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Biteko akiwasili katika kikao ili kupokea taarifa ya ujenzi wa mradi huo.
Muonekano wa Tuta kubwa, ujenbzi wa tuta hilo unaendelea.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Biteko akisikiliza maelezo kutoka kwa Emanuel Mwandambo Mhandisi Mshauri Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) kuhusu usimikaji wa mitambo mbalimbali katika eneo la Power House ambako umeme utazalishwa na kupelekwa kwenye (Swich Yard) kwa ajili ya kupoozwa na kusafirishwa kwa matumizi wakati alipotembelea mradi huo leo Septemba 16, 2023 Rufiji mkoani Pwani , ujenzi wa mradi huo kwa ujumla umefikia asilimia 91%, katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Bw. Maharage Chande.
Muomnekano wa Jengo na baadhi ya mitambo inayofungwa katika jengo la Power House.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Biteko akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) katika eneo la Power House ambapo usimikaji wa mitambo mbalimbali katika eneo hilo unaendelea, umeme utazalishwa katika eneo hilo na kupelekwa kwenye (Swich Yard) kwa ajili ya kupoozwa na kusafirishwa kwa matumizi ambapo ujenzi wa mradi huo kwa ujumla umefikia asilimia 91%, katika picha kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Bw. Maharage Chande na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Niashati Bw. Felschesmi Mramba.