Na Sophia Kingimali
Bodi ya wakurugenzi Mamlaka ya usimamizi ya wanyapori (TAWA) imesema pamoja na uhaba wa rasilimali watu katika maeneo mbalimbali ya ukaguzi wa nyara za serikali lakini wameweza kufanya Kazi kwa bidii na yenye tija kwa maslah mapana ya nchi.
Akizungumza mara baada ya kutembelea maeneo ya ukaguzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius nyerere(JNCI) ili kuona kazi ya ukaguzi inayofanywa na askari na mbwa wa mamlaka hiyo mwenyekiti wa bodi meja jenelali(mstaafu)Hamis Semfuko amesema wamejipanga kuendelea kutoa huduma ya ulinzi wa nyara za serikali na kuhakikisha usalama wake.
“Tutahakikisha Tanzania inakua salama na wanyama wetu nao wanakua Salama hivyo nitoe rai kwa wageni kuendelea Kuja na wahakikishe awavunji sheria za nchi.”amesema Meja jenelal Semfuko
Amesema kaguzi nyingi zinazofanywa katika malongo yote ya kuingilia na kutokea nchini ili kubaini uhalifu wowote huwa zinafanywa zaidi na mbwa ambao wamepewa mafunzo maalum kwa ajili ya ukaguzi wa nyara.
Akizungumzia mafunzo ya mbwa Hao amesema wamepewa mafunzo yakutambua aina mbalimbali za nyara ikiwemo meno ya Tembo.
Sambamba na hayo Meja jen.Semfuko ametoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana ikiwemo kufundishana mbinu katika ukaguzi ili zoezi Hilo liweze kufanyika kwa ufanisi mkubwa.
Akizungumza baada ya kuwapokea wajumbe wa bodi ya wakurugenzi TAWA meneja usalama na kaimu mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege Lugano Mwansasu amesema kutokana na ukubwa wa maeneo ya ukaguzi wanahitaji idadi ya askari wa wanayapori iongezwe ili kuwe na ufanisi katika ukaguzi.
Amesema kiwanja hicho cha ndege kina sehemu Sita za kazi lakini watendaji ni nane tu Hali ambayo inabidi kufanya kazi kwa mawasiliano pindi linapokea tatizo”
“Niwaombe wajumbe wa bodi mliangalie hili mtuongezee watendaji ili tuweze kufanya kazi kwa ufanisi lakini pia kuongeza mafunzo zaidi kwa mbwa ambao ni Masada mkubwa katika ukaguzi”amesema Mwansasu
Nae,afisa wanyapori mkaguzi wa nyara JNCI Sayi Nsabi ametoa ombi kwa bodi hiyo kuweza kuwapa mafunzo ya mara kwa mara wakaguzi Hao ili waweze kufanya kazi zao kiufanisi lakini pia wameomba kuweza kutengenezewa au kukunuliwa magari kwani waliyokuwa nayo yameharibika.
Kwa upende wake kaimu mkurugenzi idara ya wanyamapori wizara ya maliasili na utalii Dkt.Fortuna Msofe amesema serikali itaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha nyara za serikali zinatunzwa na kuzuia uharibifu na utoroshwaji wa nyara hizo.
Nao wahifadhi kutoka maeneo mbalimbali ya hifadhi mkoa wa Dar es salaam wamesema kuwa kutokana na juhudi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya Sita mapato ya serikali yanayotokana na utalii unaofanywa wa kutembelea maeneo ya hifadhi yameongezeka
Ziara iliyofanywa na bodi ya wakurugenzi TAWA ili lenga kuangalia namna mbwa wanavyoshiriki katika ukaguzi na utambuzi wa nyara kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori.
Ziara hiyo ilianzia katika kiwanya cha ndege cha JNIA kwa kupitia kwenye sehemu zote za ukaguzi na kuona namna ukaguzi huo unavyofanywa na mbwa kwa kushirikiana na askari.
Ambapo ziara hiyo ilitamatika katika hifadhi ya mbwa mbezi kwa kuangalia namna mbwa Hao wanavyopata mafunzo ya kutambua nyara.