Na Sophia Kingimali
Taasisi ya mama ongea na mwanao inatarajia kuanza kampeni ya nchi nzima ya kugawa viatu vya shule Kwa watoto mashuleni ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha elimu.
Akizungumza Leo Septemba 14, 2023 mwenyekiti wa taasisi hiyo Steven Mengele amesema wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kijamii ili kusapoti juhudi za serikali.
Amesema wanatarajia zoezi Hilo kuanza Kwa miikoa ya Lindi,mtwara na Ruvuma ambapo lengo ni kufikia mikoa yote nchini.
“Zoezi hili tutalifanya nchi nzima tumelenga vijijini na tutalifanya wenyewe na si kukabidhi Kwa uongozi wa shule Kwani lengo letu kuhakikisha vinamfikia mlengwa”
Amesema serikali ya awamu ya sita imeweka miundombinu mizuri katika sekta ya elimu hivyo wanawajibu kama taasisi inayounga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dkt Samia kuhakikisha watoto wanaipenda shule.
“Miundombinu imeboresha sana Sasa tunataka huyu mtoto aipende shule watoto wengi vijijini wamekuwa wakienda shule peku au na malapa hii Hali inapelekea mtoto akichomwa TU miba njiani kesho hataki Tena kurudi shule,”amesema Mengele
Aidha Mengele ametoa wito Kwa viongozi wote wa mikoa watakayopita kutoa ushirikiano ili zoezi Hilo liweze kufanikiwa.
Kampeni hiyo ilianza mwaka Jana ambapo waligawa zàidi ya viatu 2000 Kwa watoto katika mkoa ya pwani wilaya ya Kibiti na mkoa wa TABORA na wilaya zake. ambapo Sasa zoezi hilo litafanywa Kwa Kila mwezi watatembelea na kugawa katika mikoa mitatu.