Na Sophia Kingimali
Wajumbe wa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini wamepongeza juhudi za Rais Samia katika kudumisha demokrasia nchini huku wakitoa Rai Kwa serikali uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 usimamiwe na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni si Tamisemi.
Waliyabainisha hayo Leo septemba 12 wakati wa wakichangia mada iliyowakilishwa na Profesa Alexander Makulilo kuhusu Hali ya siasa nchini kuelekea uchanguzi wa serikali ya mtaa 2024 kwenye kikoa Cha kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi na hali ya siasa nchini kichofanyika jijini Dar es salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC.
Akichangia mada hiyo Mwanasiasa mkongwe, Stephen Wasira amesema amani haitakuwepo kwa sababu kutakuwa na taasisi Maalumu kwa kuwa Kuna nchi zina mahakama ya juu, tume huru lakini uchaguzi ukiisha tu amani inatoweka.
Wassira amesema amani1 ya Tanzania itadumishwa na Watanzania wenyewe kwa kupuka kauli za kuwagawa wananchi kwa kuwa hakuna demokrasia isiyokuwa na kasoro duniani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ngome ya vijana ACT-Wazalendo, Abdul Nondo amesema msingi wa amani katika demokrasia ni haki, hivyo ameshauri katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani usisimamiwe na Tamisemi bali Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama ilivyo uchaguzi mkuu.
Nae Mwenyekiti wa Diaspora, Kelvin Nyamori amesema Ili demokrasia itoe haki sawa kwa wagombea wote nyakati za uchaguzi, utaratibu wa kufanya kampeni ubadilishwe kutoka miezi miwili hadi mwaka mmoja Ili wagombea wafanye kampeni taratibu na kuwaelimisha wananchi Ili wachague viongozi wanaowajua vizuri.
Kiongozi wa madhebu ya Shia, Shehe Hemed Jalala amesema demokrasia nchini hainabudi kuheshimu haki na utu wa Watanzania kwa kutoruhusu mambo yanayokinzana na maadili, mila na desturi za Watanzania.
Mwakikishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),Dk Cammillus Kasala amesema demokrasia ya vyama vingi nchini inatekelezwa kwa shingo upande, hivyo kuna haja ya kurejesha Somo la siasa Ili wanafunzi wafundishwe misingi ya demokrasia.
Pia amesema baadhi ya viongozi wa siasa wamejiruhusu kuwa watumwa wa mambo matano ikiwemo mamlaka, faida, sifa, umaarufu na mbwembwe.
Askofu Emaus Mwamakula amesema maboresho ya sheria ya Uchaguzi yaende sambamba na maboresho ya baadhi ya vifungu vya Katiba likiwemo Kifungu cha 39(2), 75(5), 74(6) na vinginevyo na pia kianzishwe Kifungu kipya cha kuanzisha mahakama ya kuhoji matokeo ya Uchaguzi.
Nae mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM Taifa Mohammed Kawaida ametoa Rai Kwa vijana Kutoka kwenye vyama vyote vya upinzani kuchangamkia fursa zinapojitokeza Kwani rais Dkt Samia ameweka mazingira mazuri Kwa vijana na wanawake.
Akizungumza awali wakati akiwasilisha mada hiyo Profesa Alexander Makulilo amesema uchanguzi ndio njia pekee. Ya kuiweka serikali madarakani.
Amesema ili uchanguzi ufanikiwe lazima Hali ya amani na usalima izingatie lakini pia demokrasia na kufuata Sheria zinazosimamia uchanguzi.
“Amani haiji Kwa bahati mbaya imewekezwa tusibweteke Kwa kuwa nchi imekua imetajwa kuwa kusima Cha amani”amesema profesa Makulilo.
- Mkutano huo ulioandaliwa na ofisa ya msajili uliowakutanisha Baraza la vyama vya siasa na wadau wa demokrasia lengo likiwa kutathimini utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi na Hali ya siasa nchini ulifungiliwa Jana na Rais Dkt Samia unatarajiwa kufungwa kesho September 12 jijini .