Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki akizungumza jijini Dar es salaam wakati akielezea nafasi ya Tanzania waliyoipata ya kuwa mwenyeji wa Kongresi ya 50 ya Shirikisho la Vyama vya wafugaji Nyuki Duniani.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba alimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Angellah Kairuki wakati alipozungunza na waamdishi wa habari jijini Dar es Salaam Leo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akifafanua jambo katika mkutano huo.
………………………..
Serikali imewataka watanzania na wadau mbalimbali kuwekeza katika ufugaji nyuki kwa kuwa sasa uzalishaji wa asali ni tani takribani elfu 32 tu wakati kama taifa kuna uwezo wa laki 138.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumzia nafasi ya Tanzania waliyoipata ya kuwa mwenyeji wa Kongresi ya 50 ya Shirikisho la Vyama vya wafugaji Nyuki Duniani inayotarajiwa kufanyika septemba 20-25 mwaka 2027 jijini Arusha
Waziri Kairuki amesema ametumia fursa hiyo kuwataka wadau wa ufugaji nyuki nchini kutumia fursa ya mkutano huo kuvutia wawekezaji na kuongeza tija katika ufugaji na biashara nzima ya mazao ya nyuki na utalii.
Aidha Waziri Kairuki amesema kuwa kwa Tanzania kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa APIMONDIA Tanzania inakwenda kuwa nchi ya pili Barani Afrika kupewa jukumu hilo kubwa la kuandaa kongresi hiyo tangu kuanzishwa kwa APIMONDIA miaka takribani 130 iliyopita.
Awali akizungumza Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof Dos Santos Silayo amesema kuwa wamechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaweka wafugaji wa Nyuki pamoja.
Katika Mkutano huo pia amehudhuia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Wakuliyamba,Mkurugenzi wa Huduma za misitu na wadau mbalimbali.
APIMONDIA ni Shirikisho la Umoja wa Vyama vya Wafugaji nyuki Duniani lililoanzishwa mwaka 1895 nchini Italia huku. Tanzania ilijiunga katika shirikisho hilo mwaka 1984 ambapo Tanzania kwa mwaka huu nchini Chile iliibuka kuwa mshindi wa kinyanganyiro cha kuandaa Mkutano wa 50 mwaka 2027 ni Tanzania,