Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wadau wa Demokrasia kabla ya kufungua Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa Kutathmini Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi na Hali ya Siasa nchini. Mkutano huo umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba, 2023.
Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia Kutathmini Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi na Hali ya Siasa nchini katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba, 2023.
Wadau wa Demokrasia, Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa, Viongozi wa Vyama vya Siasa, pamoja na Wageni mbalimbali wakiwa kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kwa ajili ya Mkutano Maalum wa Baraza hilo na Wadau wa Demokrasia Kutathmini Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi na Hali ya Siasa nchini tarehe 11 Septemba, 2023.