Wazazi hizi chips tunazokula ni viazi tu hivyo wazazi wachungeni watoto wenu kimaadili, kwani wengi wao viazi vinawachanganya na badala yake wanaingia kwenye wimbi la mapenzi kisa wanadanganywa kwa chips tu.
Hii ni kauli iliyotolewa tarehe 9.9.2023 na Ayubu Semvua ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya shule ya msingi Turiani, iliyopo Magomeni, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Katika mahafali hayo uongozi wa shule umempongeza mdau wa maendeleo, Iddy Azan kwa namna anavyochochea maendeleo katika shule hiyo ya msingi Turiani.