Deladius Makwega – MWANZA
Wakristo wameambiwa kuwa wanatakiwa kutafakari wajibu wao kwa wengine, maana kila mmoja anawajibika kujiokoa mwenyewe na kuwaokoa na wengine, kama Yesu Kristo alivyofanya msalabani.
Huku jukumu hilo lifanyike bila ya kuchoka ili kuukamilisha Ukristo, maana siyo sahihi kupambana kujikoa mwenyewe tu.
“Nakumbuka maneno ya Katekista mmoja wakati nikiwa kijana, alisema ‘Mawazo ya Wakristo wengine ni kuwa anaweza kujiokoa peke yake, hasa kwa watu wa ndoa, utakuta mwenza anajitahidi kuokoa nafasi yake tu, yeye atasali sana, yeye atatenda matendo mema lakini mwenza wake anamuacha tu, akisema yeye ni shauri yake.’
Maneno haya yalisemwa zamani sana lakini hadi leo ninayakumbuka na ninayarudia maana yanaoana kabisa na masomo ya Misa ya Dominika ya leo, kwa hiyo masomo yote ya leo yanatuonya katika hilo.”
Hayo yamesemwa katika mahubiri ya Dominika ya 23 ya Mwaka A Liturjia ya Kanisa na Padri Zakaria Makoye ambaye ni Paroko wa Parokia ya Sumve, katika Misa ya Kwanza ya Jumapili ya Septemba 10 , 2023 katika Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Wamisionari- Parokia ya Malya, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.
Akiendelea kuhubiri katika misa hii Padri Makoye alisisitiza namna ya Wakristo wanavyotakiwa kurekibishana kama somo la injili lilivyoelekeza, huku akiwataka Wakristo kutoa michango mbalimbali iwe ya Kikanisa au Kiserikali ilimradi tu michango hiyo inasimama na kupimwa katika Sheria Mama amabyo ni Upendo.
Misa hiyo pia iliambatana na nia na maombi kadhaa,“Eee Baba Mungu, tunaomba uimarishe moyo wa umoja kati yetu, tuepekane na utengano na mafarakano, unaoletwa na mawazo mbalimbali kati yetu .”
Hadi misa hiyo ya kwanza iliyoanza saa 12 za asubuhi inamalizka, kwa ujumla hali ya hewa ya eneo zima la Malya na viunga vyae lilipata mvua kubwa tatu ambazo ziliwashawishi wakulima kuanza kupanda mashamba yao, huku wakulima wengine wakikamilisha kuyatayarisha mashamba yao,wananchi wa Malya wakiambizana kuwa sasa masika imeanza.
Mwandishi wa ripot hii ameshuhudia baadhi ya wakulima hao wakioneshana mipaka ili wakati wa kupamba wasivuke mashamba ya wenzao na kuepusha migogoro baina yao ya hapa na pale