Muonekano wa bwawa la kufua umeme la Mtera lenye uwezo wa kufua megawati 80.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji uzalishaji umeme Mha. Pakaya Mtamakaya akiwa na wabunge wa kamati ya Nishati na Madini walipotembelea bwawa la mtera
Mwenyekiti kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Ussi Salum Kondeza akipokea Maelezo kutoka kwa meneja wa kituo cha kuzalisha umeme Mtera Mha. Edmund Seif
………………..
Na Neema Mbuja
KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Leo imetembelea bwawa la Mtera ambalo ni miongoni mwa mabwawa yanayozalisha umeme nchini, kujionea namna umeme unavyozalishwa kwa njia ya maji na kuona maendeleo ya jumla ya umeme unaozalishwa kwenye bwawa hilo
Akizungumza katika ziara hiyo, mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Ussi Salum Pondeza amesema wameridhishwa na hali ya uzalishaji wa umeme kwenye bwawa la Mtera, na wamekuta mashine zote mbili zina uwezo wa kuzalisha megawati 72 huku kila moja ikizalisha megawati 38.
“Tumeridhika na uzalishaji licha ya kuwa kina cha maji kimepungua kwa kipindi hiki kutokana na kuchelewa kwa mvua ambazo zinajaza bwawa la Mtera na hivyo kusaidia uzalishaji pia kwenye mitambo ya Kidatu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uzalishaji umeme kutoka TANESCO Mha. Pakaya Mtamakaya amesema Lengo la ziara ya kamati ya Bunge ni kujionea hali halisi ya uzalishaji umeme kwenye vyanzo vya maji vya Mtera, Kidatu, na kihansi na kujipanga iwapo mvua za kiwango cha juu zitanyesha kama ilivyotangazwa na mamlaka ya hali ya hewa hivi karibuni.
” kwa Kawaida huwa tunapata mvua Mara mbili kwa msimu na iwapo msimu ukichelewa husababisha uhaba wa maji, lakini kwa sasa hauathiri upatikanaji wa umeme kwani kuna vyanzo mbadala vya uzalishaji, alisema Pakaya.
Bwawa la Mtera ni miongoni mwa mabwawa kongwe nchini lenye uwezo wa kuzalisha megawati 80.