Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na watumishi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao kilicholenga kujadili utekelezaji wa majukumu ya idara hiyo.
Watumishi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao kilicholenga kujadili utekelezaji wa majukumu ya idara hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya idara yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao kilicholenga kujadili utekelezaji wa majukumu ya idara hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza jambo na Naibu Waziri, ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Ndugange wakati wa kikao kazi cha Mhe. Mchengerwa na watumishi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais-TAMISEMI kilicholenga kujadili utekelezaji wa majukumu ya idara hiyo.